Mstahiki Meya wa Jiji la Mwanza, Costantine Sima ametoa muda wa masaa 24 kwa mfanyabiashara Sajady Ahmad awe amevunja jengo alilolijenga katika Mtaa wa Nera bila kufuata taratibu.
Meya Sima ametoa agizo hilo mapema Januari 08, 2020 akiwa ameambatana na viongozi mbalimbali jijini Mwanza, baada ya kufika katika eneo la jengo hilo lililopo katika kiwanja namba 15 block B mali ya Chama cha Mapinduzi (CCM).
Alisema baada ya mfanyabiara huyo kupata idhini ya kuwekeza katika eneo hilo, alianza ujenzi bila kuwa na vibali pamoja na kukiuka sheria ya mipango miji inayotaka maeneo ya katikati ya Jiji kujengwa majengo ya ghorofa na si majengo mafupi kama alivyofanya.
Aidha aliongeza kuwa Disemba 03, 2020 mfanyabiashara huyo alipokea barua ya kusitisha ujenzi huo lakini alikaidi na kuendelea hadi hatua ya upauaji aliyofikia sasa na kwamba akishindwa kubomoa hilo Halmashauri ya Jiji la Mwanza italibomoa na kisha atalipa gharama za ubomoaji.
Katika hatua nyingine Meya Sima aliwaonya wale wote wanaoendelea na ujenzi wa majengo mbalimbali bila kuwa na vibali kutoka Halmashauri ya Jiji la Mwanza na kueleza kuwa zoezi la ukaguzi wa majengo yasiyo na vibali litaendeshwa muda hivi karibuni.
Barabara ya Balewa
Sanduku la Posta: 1333,Mwanza
Simu: +255 28 250 1375
Simu ya Kiganjani: 0755741738
Barua Pepe: cd@mwanzacc.go.tz
Copyright ©2017 Mwanza City Council . All rights reserved.