Mbunge wa Nyamagana Mhe. Stanslaus Mabula amefanya ziara ya kukagua shule za sekondari kwa lengo la kufanya tathimini na kujua mapungufu ili kuyafanyia kazi ikiwa nisehemu ya utekelezaji wa ilani ya Chama Cha Mapinduzi.
Katika ziara hiyo Mhe.Mabula amezuru shule nne za Sekondari ambazo ni Nyamagana, Fumagira, Stanslaus Mabula, na Mahina.
Mhe.Stanslaus Mabula akiwa katika ziara yake ameeleza kuwa Nyamagana ni moja ya wanufaika waliyopata takribani Bilioni 3 na milioni 900 kwa ajili ya ujenzi wa Madarasa na kukarabati wa miundombinu mingine.
Kupitia ziara hiyo, Mbunge wa Nyamagana aipongeza TASAF kwa mchango wake mkubwa wa ujenzi wa miundombinu licha ya kusaidia kaya masikini lakini pia imetambua changamoto inayowakabili wanufaika wao ikiwa ni pamoja na ujenzi wa madarasa, pia amewapongeza watendaji wa mtaa na kata kwa kuhakikisha wanachangia 10% ya ujenzi na uboreshaji wa miundombinu ya madarasa na kusisitiza kuwa mchango huo wanaoutoa wananchi kuuainisha ili nguvu kazi yao ionekane kwenye makabidhiano pindi mradi unavyokamilika na kuwasilishwa.
Aidha Mbunge wa Nyamagana akiwa katika eneo la shule ya Sekondari ya Stanslaus Mabula amesema Serikali italeta viti na Meza kwa walimu na kueleza kuwa Milioni 481 zilizopo zitajenga Mabweni 2, Madarasa 4, Nyumba za waalimu na Matundu ya vyoo 10. Vilevile ameongeza kuwa atawatuma wataalam wa umeme na maji kuleta huduma hizo mara moja na mara baada ya umeme kuletwa itanunuliwa mashine yakutolea kopi lakini pia kuhakikisha miundombinu ya shule hiyo inakaa sawa ili kuharakisha uanzishwaji wa kidato cha Tano na Sita.
Naye, Ndg Mafuru Afsa Elimu Sekondari Wilaya ya Nyamagana.Amempongeza Mbunge na serikali kwa ujumla kwa jitihada wanazozifanya ili kuhakikisha Halmashauri ya Jiji la Mwanza inapata shule ya kidato cha Tano na Sita ya mfano nakuongeza kuwa shule hiyo Stanslaus Mabula itakapofunguliwa itakuwa ni moja kati ya shule bora za Serikali katika Wilaya ya Nyamagana.
Mbunge wa Nyamagana amehitimisha kwa kuwataka watendaji wa mtaa na kata kwa kushirikiana na Madiwani kulinda maeneo ya Shule yasiingiliwe na wananchi na kwa yeyote atakaekaidi na kukiuka maagizo ya uongozi achukuliwe hatua za kisheria.
Barabara ya Balewa
Sanduku la Posta: 1333,Mwanza
Simu: +255 28 250 1375
Simu ya Kiganjani: 0755741738
Barua Pepe: cd@mwanzacc.go.tz
Copyright ©2017 Mwanza City Council . All rights reserved.