Halmashauri ya Jiji la Mwanza na Manispaa ya Wilaya ya Ilemela wameshiriki Mafunzo ya Usimamizi wa Mapato ya ndani yanayofanyika kwa siku 4 katika ukumbi Wa Mandela - Gold Crest kuanzia tarehe 22April, hadi 25April,2024 yaliyobeba dhima ya kuziwezesha Halmashauri hizo kusimamia kwa weledi ukusanyaji mapato ya ndani ya Halmashauri hizo.
Mafunzo hayo yaliyodhaminiwa na GREEN AND SMART CITIES yamehusisha Washiriki kutoka Idara na Vitengo mbalimbali kama vile Tehama, Sheria, Mapato , Ardhi, Mifugo, Uvuvi, Kilimo, Uchumi, Habari, Biashara na Uwekezaji pamoja na Idara ya Ujenzi.
Akifungua rasmi Mafunzo hayo Eng. Anthony Sanga kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. Said Mtanda Amesema "Sekretarieti ya Mkoa wa Mwanza inatarajia kuona kwamba baada ya Mafunzo haya kutakuwa na maongezeko makubwa kutoka makusanyo ya awali yaliyokuwa yakipatikana ndani ya Halmashauri zetu zote mbili yaani Mwanza Jiji na Manispaa ya Halmashauri ya Ilemela."
Aidha, Eng. Sanga ameongeza kusema kuwa tunataraji kuona kuwa kumekuwepo na ubunifu mpya wa kubuni vyanzo vipya vya mapato, kuimarisha Mikakati na mbinu za kukusanya mapato, kuweka sheria ndogo za ukusanyaji mapato hayo na kuzisimamia, kulinda nidhamu ya mapato yanayopatikana, kujenga miundombinu hasa katika maeneo ambayo mazao ya Samaki yatawekwa sambamna na machinjio ya mifugo, pamoja na kuanzisha Kanzidata kwa ajili ya kudhibiti makusanyo yanapatikana.
Naye Mwezeshaji wa Mfunzo hayo Prof. Thomas Mhanga amewataka Washiriki wote wa Mafunzo hayo kushiriki kikamilifu katika mafunzo hayo ikiwa ni pamoja na kuchangia mawazo panapo stahili ili kuongeza uelewa zaidi kwa washiriki wote.
Barabara ya Balewa
Sanduku la Posta: 1333,Mwanza
Simu: +255 28 250 1375
Simu ya Kiganjani: 0755741738
Barua Pepe: cd@mwanzacc.go.tz
Copyright ©2017 Mwanza City Council . All rights reserved.