Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Umoja wa Wanawake Tanzania Ndg, Suzan Peter Kunambi (MNEC)amefanya ziara ya ukaguzi wa miradi ya kimkakati katika Wilaya ya Nyamagana leo Agosti 12,2024 huku akitaka kujua namna Ilani ya Chama Cha Mapinduzi inavyotekelezwa
Katika ziara hiyo Ndg, Suzan Peter Kunambi (MNEC) Amekagua na kuzindua Mradi wa vyerehani Katika Ofisi za Ccm wilaya ,unaomilikiwa na Umoja wa Wanawake Mwanza, ambao walifadhiliwa na Mbunge wa Viti maalum Mhe Kabula Shitobero, licha ya uzinduzi huo kufana wamiliki wameshauriwa kuukuza mradi huo kwa kuwaomba wengine kuongeza vyerehani vya kisasa na kuhakikisha wanakuwa na mhasibu watakaemuamini kwenye suala la pesa ili kuondoa migogoro inayohusiana na mradi huo.
Ndg,Suzan Peter Kunambi (MNEC) ambaye ni Katibu Mkuu Jumuiya ya Wanawake Tanzania (UWT)ameweza kukagua miundombinu ya Shule ya sekondari Stanslaus Mabula yenye jumla ya wanafunzi 82 na Shule ya Msingi Kanenwa zilizopo kata ya Kishiri, nakuwapongeza waliyosimamia miradi kwani imekamilika vizuri pasipo na shaka huku akizitaja kuwa shule bora za mfano nakuwahimiza wazazi kuwasomesha watoto kwakuwa serikali imewasogezea wanachi miundombinu ya shule karibu huku pia akiwaambia wanafunzi waitunze kwa kuwa itatumika kizazi na kizazi .
Pia Ndg, Suzan Peter Kunambi (MNEC) amewataka wananchi wa Kishiri, kujitokeza kujiandikisha kwenye uboreshaji wa Daftari la kupiga kura linalotarajia kuanza Agosti 21-28 , 2024 huku akisisitiza anaetakiwa kujiandikisha ni Mwenye Miaka 17 nakuendelea na amewataka wanawake kujitokeza kugombea nafasi mbalimbali katika serikali huku akisisitiza waoneshe uthubutu na uwezo wao.
Naye, Meneja Tarura Jiji la Mwanza Ndg, Dastani kishaka amewasilisha taarifa ya ujenzi wa Barabara ya kiwango cha lami inayojengwa Buhongwa -Igoma yenye urefu wa Km 14.4 na ujenzi umefikia asilimia 45 na unagharimu kiasi cha bilioni 22.7 bila VAT na unakaribia kukamilika tarehe 29 Feb, 2025 naKatibu Mkuu wa umoja wa Wanawake Tanzania (UWT)baada ya kupokea taarifa hiyo amesisitiza mradi usimamiwe na kuisha kwa wakati ili kufungua fursa kwakuwa itakuwa chachu ya maendeleo kwa watanzania.
Mbunge wa viti Maalum Mhe, Kabula Shitobero amewataka wazazi kuwajibika katika Malezi, ili kukomesha vitendo vya unyanyasaji wakijinsia huku akisema kati ya watoto 3 wa kike 1 kafanyiwa ukatili wa kijinsia na katika 7 wakiume 1 kafanyiwa ukatili hivyo basi amesisitiza wazazi kutowapa watoto vitu hatarishi kama simu vinavyopelekea mmomonyoko wa maadili na kuacha Tamaduni zilizopitwa na wakati na kutoa taarifa kunakohusika pindi tu mtoto anapofanyiwa unyanyasaji wa kijinsia.
Ndg, Suzan Peter kunambi (MNEC) amewataka wananchi kuchangamkia fursa za Mikopo ya 10% inayotolewa kwa wanawake 4% , vijana 4% na walemavu 2% ambapo mpaka sasa kuna zaidi ya Billioni mbili kwa ajili ya mikopo kwenye Halmashauri ya Jiji la Mwanza, hivyo amesisitiza watu wapewe elimu nawakipeswa ili kupunguza mikopo inayoumiza wananchi.
Wananchi wametakiwa kujikita katika matumizi ya Nishati safi ya kupikia. ikiwa ni mpango wa Rais Dr, Samia Suluhu Hassan ili kuondoa uchafuzi wa mazingira, Moshi wa muda mrefu unaopelekea kuoza kwa mapafu hivyo kuja na sera hiyo ambayo utekelezaji wake unaenda hadi 2035 ili kuhakikisha kila mwananchi anajikita katika nishati safi.
Barabara ya Balewa
Sanduku la Posta: 1333,Mwanza
Simu: +255 28 250 1375
Simu ya Kiganjani: 0755741738
Barua Pepe: cd@mwanzacc.go.tz
Copyright ©2017 Mwanza City Council . All rights reserved.