Mkuu wa wilaya ya Nyamagana Mhe, Amina Makilagi akiwa ameambatana na Wajumbe wa Kamati ya Usalama na Wakuu wa Idara kukagua miradi mbalimbali ameridhishwa na kasi ya ujenzi wa Barabara ya Buhongwa -Igoma
Aidha Meneja TARURA , Muhandisi Dastani Alifred ambaye ni msimamizi wa mradi amesema tunajenga Barabara kwa viwango vinavyohitajika na mkandarasi anapaswa kumaliza kwa wakati kwa
sababu fedha za ujenzi zipo licha yakuomba kuongezewa mkataba kama akikidhi vigezo ataongezewa asipokidhi itabidi apigwe faini ya (re -created demages)kwa kushindwa kumaliza mradi.
Mbali na kukagua barabara Mkuu wa wilaya na wajumbe wa kamati ya Usalama wamehitimisha ziara hiyo kwa kukagua ujenzi wa Shule ya Sekondari Fumagila unaogharimu kiasi cha shilingi 175,000,000 na ujenzi wa Mabweni mawili , Madarasa 4 na Nyumba 2 za waalimu katika Shule ya Sekondari Stanslaus Mabula wenye gharama ya shilingi 581,000,000. Buhongwa -Kishiri hadi Igoma .
Ziara hiyo ya siku mbili imeanza Februari 13-14, 2025 kwa lengo la kukagua utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo wilayani humo.
Katika ziara hiyo Kamati ya Usalama wamekagua ujenzi wa mradi wa Barabara ya km 14.4 unaojengwa na Mkandarasi Zong-Mei Engeneering group Company Limted kwa kiwango cha rami kutoka Buhongwa, Kishiri hadi Igoma unaogarimu kiasi cha shilingi Bilioni 22.7
Mhe Makilagi amempongeza Mkandarasi anayejenga Barabara ya Buhongwa,kishiri hadi Igoma kwa kasi anayoenda nayo licha ya kuchelewa kuanza ujenzi 20 Nov, 2023. Lakini hadi sasa wamefikia asilimia 71% na kumtaka kuongeza kasi ili ujenzi uishe kwa wakati.
Ameongeza kuwa kukamilika kwa Barabara hiyo kunaimarisha uchumi, kuna rahisisha maisha ya watu katika kupata huduma za kijamii, na kisiasa nakutoa wito kwa mkandarasi kumaliza haraka ili izinduliwe kabla ya uchaguzi mkuu .
Pia Mhe. Makilagi ametoa maelekezo kwa Mkandarasi, kuhakikisha wanajenga uzio kwenye shule zote ambapo Barabara inapita kulingana na mkataba unavoelekeza nakuweka alama kuonesha kuwa maeneo hayo kuna taasisi ili kuzuia ajari Barabarani.
Barabara ya Balewa
Sanduku la Posta: 1333,Mwanza
Simu: +255 28 250 1375
Simu ya Kiganjani: 0755741738
Barua Pepe: cd@mwanzacc.go.tz
Copyright ©2017 Mwanza City Council . All rights reserved.