Kamati ya Siasa ya Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Mwanza yafanya ziara ya kukagua utekelezaji wa Ilani kwa Mwaka wa Fedha 2020/2021 leo 24/8/2021 katika Halmashauri ya Jiji la Mwanza
Akiongoza ziara hiyo Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mwanza Dr Antony Diallo akiambatana na Mkuu wa Mkoa Mhandisi Robert Gabriel, Katibu wa CCM Mkoa Ndugu Julius Peter, MNEC wa CCM mkoa Ndugu Jamal Babu, MNEC Richard Bundala na Wajumbe wote wa Kamati ya siasa mkoa wa Mwanza
Wametembelea na kukagua Miradi mbalimbali inayotekelezwa na Serikali ya chama cha mapinduzi katika halmashauri ya jiji la Mwanza
Miradi hiyo ni Eneo la Ufukweni mwa ziwa Victoria linalojengwa na TAMPERE katika kata ya Isamilo.
Ujenzi wa Soko kuu Mjini Kati,
Kutembelea na kuona ukarabati wa Shule Kongwe za Pamba Sekondari na Mwanza Sekondari. Ambapo ukarabati wa hizo shule mbili umegarimu zaidi ya Bilioni 1 kutoka serikali kuu .
Kamati ya siasa imeshuhudia Walimu wakiipongeza Serikali ya awamu ya sita inayo ongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan Kwa kuendelea kutoa fedha za ujenzi na ukarabati wa majengo, Upandishaji wa Madaraja ya walimu
Aidha Wamemuomba Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Mwanza Dr Antony Diallo kuwafikishia salamu hizo kwa Mwenyekiti wa CCM Taifa Mama Samia Suluhu Hassan
Hata hivyo Kamati imetembelea na na Kuona Ujenzi wa Meli Mpya ya MV- MWANZA HAPA KAZI TU ambayo imefikia katika hatua nzuri ya asilimia 60 ya Ujenzi.
Aidha Kamati imetembelea ujenzi wa soko kuu la kisasa pamoja na ujenzi wa stendi ya Nyegezi ambapo Mkandarasi ameahidi kufikia Mwakani mwezi Juni miradi itakuwa imekamilika.
Pia wajumbe Wametembelea na kuona ujenzi wa Bweni la watoto wenye Mahitaji Maalumu ya Shule ya msingi Buhongwa 'A'_
Barabara ya Balewa
Sanduku la Posta: 1333,Mwanza
Simu: +255 28 250 1375
Simu ya Kiganjani: 0755741738
Barua Pepe: cd@mwanzacc.go.tz
Copyright ©2017 Mwanza City Council . All rights reserved.