• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua Pepe |
    • Malalamiko |
Mwanza City Council
Mwanza City Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Jiji la Mwanza

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Orodha ya Viongozi Waliopita
      • Wenyeviti wa Halmashauri
      • Wakurugenzi
      • Wakuu wa Wilaya
    • Dhima na Dira
    • Maadili ya msingi
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Kilimo na Ushirika
      • Maendeleo ya Jamii
      • Uchumi, Mipango na Ufuatiliaji
      • Mazingira na Usafi
      • Fedha na Biashara
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mifugo na Uvuvi
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Maji
    • Vitengo
      • TEHAMA,Habari na Uhusiano
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Sheria na Usalama
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Nyuki
  • Fursa za Uwekezaji
    • Maeneo ya uwekezaji
    • Vivutio vya utalii
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Usafi wa mazingira na uhifadhi wa taka ngumu
    • Leseni
    • Kilimo
    • Mifugo na Uvuvi
    • Maji
  • Baraza la Madiwani
    • Orodha ya madiwani
    • Kamati za kudumu za halmashauri
    • Ratiba ya vikao
    • Mihtasari ya vikao vya baraza
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi inayoendelea
    • TASAF
    • Mfuko wa Jimbo
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu za Maombi
    • Waraka
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Maktaba ya Video
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio Yajayo
    • Magazine

Kamati ya Siasa Mkoa wa Mwanza yaridhishwa na mpangilio wa ujenzi unaoendelea wa soko kuu la kisasa jijini Mwanza.

Posted on: September 1st, 2022


Hayo yamebainishwa mapema leo Septemba Mosi wakati wa ziara ya Kamati ya siasa Mkoa wa Mwanza walipotembelea mojawapo ya mradi mkakati unaotekelezwa wa ujenzi wa soko kuu la kisasa la mjini kati katika Halmashauri ya Jiji la Mwanza.


"Mimi binafsi nimeridhishwa sana na mpangilio wa mradi huu ni jumuishi umegusa makundi karibu yote kuna sehemu ya machinga na mama lishe na uwekezaji huu unakwenda kuifanya mwanza kuwa ya kisasa na kuifananisha na majiji mengine." Amesema Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mhe. Adam Malima ambaye pia ni Kamisaa wa Kamati ya siasa Mkoa.


Mhe Malima emeongeza kuwa mradi huu mkubwa unaogharimu zaidi ya Bilioni 20 hadi kukamilika kwake una nia ya kuhamisha maisha ya wananchi kwenda kuwa ya kisasa na kutoa rai kwa halmashauri, huduma zitakazotolewa ma soko hili ziwe zilenge kuwasaidia wananchi hasa wafanyabiashara wadogo ambao Mhe. Rais amekua akiwahangaikia."


Kwa upande wake, Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Mwanza Ndg. Erick Mvati  amefafanua kuwa mradi huu ambao umeanza Oktoba 2020 na unatarajia kukamilika ifikapo  Septemba 30, 2022 unagharimu zaidi ya  Tshs. Bilioni 20 hadi kukamilika kwake  na kwa sasa umefikia asilimia 79 ya utekelezaji.


Aidha, amefafanua kuwa Mradi huo ulioajiri zaidi ya vijana 100 wakati wa utekelezaji, utasaidia kuongeza mapato ya Halmashauri na kupunguza utegemezi kutoka Serikali kuu kutokana na huduma kadhaa zitakazokuwemo zikiwemo mabenki, vizimba vya wafanyabiashara wadogo, eneo la wafanyabiashara wakubwa, michezo ya watoto na eneo la kuegesha magari zaidi ya 150.


Ikiwa katika Halmashauri ya Jiji la Mwanza, Wilaya ya Nyamagana, Kamati imepata nafasi pia ya kupita na kukagua  bandari ya Mwanza Kusini na kukagua Ujenzi wa Meli kubwa ya kisasa ya MV Mwanza ambayo inatekelezwa na Mkandarasi Gas Entec ya Nchini Korea kwa Bilioni 70 na imesisitiza uharakishwaji wa ujenzi huo kwa manufaa ya wananchi waishio kwenye ukanda wa maziwa makuu.


"Ujenzi wa hii Meli ulianza January 2019 na ulikua uende kwa miaka miwili lakini zilitokea changamoto nyingi ambapo mkataba uliongezwa hadi mwezi Mei 2023 ambapo kwa sasa umefikia asilimia 71 ya ujenzi na hakuna meli kubwa kama hii kwenye ukanda wa maziwa makuu." Amefafanua Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Huduma za Meli, Erick Hamis


Bwana Hamis ameongeza kuwa Meli hiyo inajengwa na watanzania zaidi 200 na wataalamu kutoka nje wapo 6 tu na ifikapo mwezi wa 10 mwaka huu meli hii itaingizwa kwenye maji ambapo matengenezo mengine yataendelea ikiwa kwenye maji.

Matangazo ya Kawaida

  • TANGAZO KWA WAOMBAJI AMBAO HAWAJAWASILISHA TAARIFA ZAO KWA AJILI YA MNADA April 30, 2025
  • JITOKEZE KUJIANDIKISHA October 16, 2024
  • TANGAZO LA UPANGISHAJI WA MAENEO YA BIASHARA KATIKA SOKO KUU December 14, 2024
  • TANGAZO LA KUPEWA NA KUINGIZWA KATIKA MFUMO WA TAUSI -UPANGISHAJI WA SOKO KUU MWANZA February 21, 2025
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • WAKILI KIBAMBA ASISITIZA NIDHAMU ENEO LA KAZI

    May 08, 2025
  • WAWEZESHAJI WATOA MBINU ZA UFUNDISHAJI WA SOMO LA KIINGEREZA KUONGEZA UFAULU NYAMAGANA

    May 05, 2025
  • WAJUMBE WA MABARAZA YA KATA WATAKIWA KUTIMIZA WAJIBU WAO KWA HAKI

    March 26, 2025
  • DC NYAMAGANA MTAA KWA MTAA KUSIKILIZA KERO ZA WANANCHI

    March 28, 2025
  • Tazama Zote

Video

Maadhimisho ya wiki ya utumishi wa Umma Halmashauri ya Jiji la Mwanza
Video Zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Fomu Mbalimbali
  • Kuhusu Sisi

Viunganishi Linganifu

  • Tovuti ya Mkoa wa Mwanza
  • Vibali Kusafiri nje ya Nchi
  • ESS(Watumishi Portal)
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Idara Kuu ya Takwimu(NBS)

Watembeleaji

world map hits counter

Idadi ya wageni

freevisitorcounters's Website

Ramani Elekezi

Wasiliana Nasi

    Barabara ya Balewa

    Sanduku la Posta: 1333,Mwanza

    Simu: +255 28 250 1375

    Simu ya Kiganjani: 0755741738

    Barua Pepe: cd@mwanzacc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Eneo

Copyright ©2017 Mwanza City Council . All rights reserved.