Kamati ya Huduma,Uchumi,Afya na Elimu ya Halmashauri ya Jiji la Mwanza leo imefanya ziara ya kikazi kuangalia utekelezaji wa miradi mbalimbali ya utoaji huduma na ukuzaji Uchumi kwa wananchi .
Kamati hiyo ikiongozwa na Mhe. Hamidu Seleman ambaye ni mwenyekiti wa kamati wametembelea Soko kuu la Mwanza kuangalia eneo litakapojengwa soko jipya la kisasa, Eneo la Sinai - mahali ambapo wajasiriamali wadogo wanatarajiwa kuamishiwa kupisha ujenzi wa Soko kuu, Ujenzi wa madarasa matatu shule ya msingi Kiahiri, ujenzi wa matundu ya vyoo shule ya msingi Lwanhima ujenzi wa madarasa matano Buhongwa sekondari na ujenzi wa nyumba za walimu shule ya msingi Iseni.
Aidha Kamati ilipata fursa ya kutembelea Zahanati ya Buhongwa kuona namna wananchi wanavyohudumiwa.
Kwa kuhitimisha ziara Mwenyekiti na Kamati nzima wameridhishwa kwa namna miradi inavyotekelezwa lakini pia wamevutiwa ubunifu wa Halmashauri kununua mashine ya matofali inayosaidia kwa kiasi kikubwa ujenzi wa madarasa kwa kasi katika shule mbalimbali Jijini Mwanza.
"Sasa hivi wananchi wameitikia kuchangia maendeleo katika kata zote hivyo tunamwomba Mkurugenzi aanze kuleta matofali ili wananchi wa maeneo haya waweze kuchangia zaidi" Mhe Diwani wa kata ya Kishiri alisikika akisema.
Madarasa mapya ya shule ya Sekondari Buhongwa yaliyoanza kujengwa mwezi Februali 2019
Jengo la madarasa matatu yanayojengwa kwa nguvu za wananchi wakishirikiana na Halmashauri ya Jiji la Mwanza Kishiri shule ya msingi.
Msingi wa madarasa mawili uliojengwa na wananchi wa Buhongwa ukiwa kwenye hatua za kukamilika.
Soko la nguo mlango mmoja linalokadiriwa kugarimu milioni 171 mpaka kukamilika likiwa kwenye asilimia 60 katika ujenzi.
Barabara ya Balewa
Sanduku la Posta: 1333,Mwanza
Simu: +255 28 250 1375
Simu ya Kiganjani: 0755741738
Barua Pepe: cd@mwanzacc.go.tz
Copyright ©2017 Mwanza City Council . All rights reserved.