Naibu Meya wa Jiji la Mwanza Mhe; Bikhu Kotecha ameiongoza Kamati ya Fedha na Uongozi ya Halmashauri ya Jiji la Mwanza katika ziara ya ukaguzi wa miradi ya maendeleo yenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni mbili.
Akizungumza na viongozi mbalimbali wa serikali na Kamati za usimamizi wa miradi hiyo,Mhe; Kotecha amewataka viongozi hao kuhakikisha wanatekeleza na kukamilisha utekelezaji wa miradi hiyo Kwa wakati na pia kuzingatia thamani ya fedha (value for money).
Kotecha amaesema lengo la serikali ni kuhakikisha wananchi wanasogezewa huduma karibu kama ambavyo serikali ya awamu ya sita imekuwa ikiahidi jamii katika utekelezaji wa shughuli zake.
Akitoa shukrani zake Kwa serikali ya awamu ya sita,diwani wa kata ya Luchelele Mhe; Vincent Lusana Tegge amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan Kwa kuleta fedha ya ujenzi wa shule mpya ya sekondari Kisoko na pia kuushukuru Uongozi wa Halmashauri ya Jiji la Mwanza Kwa kukubali utekeleza mradi wa ujenzi wa shule hiyo kupitia vikao vya Kamati na Mabaraza ya Madiwani.
Tegge amesema ujenzi wa shule hiyo mpya utasaidia kuboresha elimu na pia kuwapunguzia wanafunzi umbali mrefu wa kupata elimu hasa ikizingatiwa kuwa kata ya Luchelele yenye mitaa kumi Kwa sasa inahudimiwa na shule Moja tu ya Luchelele yenye kidato Cha kwanza hadi Cha nne.
Kamati ya Fedha na Uongozi imetembelea na kukagua jumla ya miradi minne ya maendeleo ambayo utekelezaji wake unaendelea ikiwamo ujenzi wa shule mbili mpya za sekondari za Kisoko na Kakebe na pia upanuzi wa zahanati mbili za Mhandu na Mahina ambapo miradi yote hii inagharimu zaidi ya shilingi bilioni mbili.
Barabara ya Balewa
Sanduku la Posta: 1333,Mwanza
Simu: +255 28 250 1375
Simu ya Kiganjani: 0755741738
Barua Pepe: cd@mwanzacc.go.tz
Copyright ©2017 Mwanza City Council . All rights reserved.