Halmashauri ya Jiji la Mwanza Tunakushukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, tumefaidika na fedha zinazotokana na tozo za miamala ya Simu.
Tshs mil 250 Ujenzi wa Kituo cha Afya Bulale, kilichopo kata ya Buhongwa tumekamilisha kwa asilimia 100.
Akipokea kituo hicho, Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhandisi Robert Gabriel amesema, uwepo wa Jengo la Mama na Mtoto ni jibu sahihi la kuhakikikisha Mwanamke mwingine na Mtoto hawafi kutokana na ujauzito,
Na mama unapokua mjamzito njoo kituo cha afya katika hatua za awali utapewa huduma za afya toka mwanzo ili kuhakikisha mtoto anakua salama.
Mhe. Mkuu wa Mkoa pia amepongeza Halmashuri kwa kubakiza chenji kiasi cha takribani mil. 14 katika mradi huu
'Niwapongeze kwa kubakisha chenji na hiyo dhamira isirudi nyuma na tukalete utamaduni kwamba ujauzito siyo ugonjwa, siyo balaa, tuwalete wajawazito walio maeneo yetu waje wapate huduma ili wajifungue salama.
Kama mkoa tumeandaa kauli mbiu
'Maisha ya Mama Mjamzito na mtoto yapo mikononi mwangu, tuwajibike kwa pamoja kuwavusha salama'
Utekelezaji wa ujenzi wa Kituo cha Afya Bulale umejumuisha jengo la maabara, Wodi ya wazazi, mashimo ya maji taka na kichomea taka.
Barabara ya Balewa
Sanduku la Posta: 1333,Mwanza
Simu: +255 28 250 1375
Simu ya Kiganjani: 0755741738
Barua Pepe: cd@mwanzacc.go.tz
Copyright ©2017 Mwanza City Council . All rights reserved.