• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua Pepe |
    • Malalamiko |
Mwanza City Council
Mwanza City Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Jiji la Mwanza

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Orodha ya Viongozi Waliopita
      • Wenyeviti wa Halmashauri
      • Wakurugenzi
      • Wakuu wa Wilaya
    • Dhima na Dira
    • Maadili ya msingi
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Kilimo na Ushirika
      • Maendeleo ya Jamii
      • Uchumi, Mipango na Ufuatiliaji
      • Mazingira na Usafi
      • Fedha na Biashara
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mifugo na Uvuvi
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Maji
    • Vitengo
      • TEHAMA,Habari na Uhusiano
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Sheria na Usalama
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Nyuki
  • Fursa za Uwekezaji
    • Maeneo ya uwekezaji
    • Vivutio vya utalii
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Usafi wa mazingira na uhifadhi wa taka ngumu
    • Leseni
    • Kilimo
    • Mifugo na Uvuvi
    • Maji
  • Baraza la Madiwani
    • Orodha ya madiwani
    • Kamati za kudumu za halmashauri
    • Ratiba ya vikao
    • Mihtasari ya vikao vya baraza
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi inayoendelea
    • TASAF
    • Mfuko wa Jimbo
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu za Maombi
    • Waraka
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Maktaba ya Video
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio Yajayo
    • Magazine

HOSPITALI YA NYAMAGANA YANUFAIKA NA VIFAA KUTOKA WURZBURG – UJERUMANI

Posted on: December 1st, 2023

Mstahiki Meya wa Jiji la Mwanza Ndg. Sima Costantine Sima kwa niaba ya Wananchi, Madaktari na Wauguzi wa Hospitali ya Wilaya ya Nyamagana Jijini Mwanza, amepokea vifaa tiba kutoka Jiji la Wurzburg nchini Ujerumani tarehe 01 Desemba,2023 vyenye thamani ya shilingi milioni 115. kwa ajili ya huduma ya wodi ya Watoto wachanga (Neonatal) ikiwa ni matokeo mazuri ya mahusiano mema yaliyopo kati ya Mji wa Mwanza na Mji wa Wurzburg- Ujerumani.

Awali kabla ya makabidhiano hayo, Mganga Mkuu wa Hospitali ya wilaya ya Nyamagana Dkt. Pima Sebastian alieleza kuwa Hospitali hiyo haikuwa na Kitengo maalum cha huduma kwa ajili ya Watoto wachanga hivyo kwa kushirikiana na Jiji Rafiki la Wurzburg- Ujerumani waliona vema kuanzisha rasmi kitengo hicho na hivyo kufanikisha kupata vifaa tiba ambavyo ni:- Ultrasound 2, Babywormers 5, na vifaa vingine muhimu kwa ajili ya wodi ya Watoto.

Aidha Dkt. Pima amesema “ Madaktari Pamoja na wauguzi 40 watapatiwa mafunzo ya namna nzuri ya kutumia vifaa hivyo ambapo madaktari na wauguzi 20 tiyari wamepata mafunzo hayo na wengine 20 watapatiwa mafunzo pia ili kwa Pamoja huduma hii kwa Watoto iweze kuboreka Zaidi.”

Kwa upande wake Ndg. Billy Brown ambaye ni Mratibu wa Miji Dada katika Halmashauri ya Jiji la Mwanza ameeleza furaha kubwa aliyonayo kwa mahusiano mazuri kati ya Jiji la Mwanza na Jiji la Wurzburg yaliyoanza tangu mwaka 1966 na kwamba kupitia mahusiano hayo miradi mingi imetekelezeka ukiwemo sasa huu wa vifaa tiba kwa ajili ya wodi ya Watoto wachanga katika hospitari yetu ya wilaya ya Nyamagana.

Akihitimisha shughuli hiyo ya mapokezi ya vifaa tiba hospitalini hapo, Mstahiki Meya Ndg. Sima ametoa shukrani za dhati kwa niaba ya Wananchi na Madaktari  wa Wilaya ya Nyamagana kwa Meya wa Jiji la Wurzburg Ndg. Christian Schuchardt akiwakilishwa na Ndg. Dominick Weshofern na Bi. Anuschka Heid kwa kuona umuhimu juu ya jambo hili muhimu; huku akiwataka madaktari na wauguzi hospitalini hapo kuvitumia na kuvitunza vema vifaa hivyo ili viendelee kutufaa Zaidi kwa mahitaji ya huduma za Watoto wachanga.

Matangazo ya Kawaida

  • TANGAZO LA RATIBA YA KUINGIA KWA WAPANGAJI WA MAENEO MBALIMBALI YA SOKO KUU. June 29, 2025
  • TANGAZO LA MAPENDEKEZO YA SHERIA NDOGO ZA HALMASHAURI YA JIJI LA MWANZA July 10, 2024
  • MATOKEO YA USAILI WA KUANDIKA (MCHUJO) KADA YA MSAIDIZI WA KUMBUKUMBU DARAJA LA II - MWANZA JIJI April 29, 2023
  • KUITWA KAZINI NAFASI YA MEO III, MWANDISHI MWENDESHA OFISI II, RMA II na DEREVA II January 08, 2024
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • HALMASHAURI YA JIJI LA MWANZA KWA KUSHIRIKIANA NA RAILWAY CHILDREN AFRICA YAPANGA MIKAKATI YA KUKABILIANA NA WATOTO WA MTAANI

    June 26, 2025
  • HANANG' WAJIFUNZA MBINU ZA KUONGEZA MAPATO KUTOKA HALMASHAURI YA JIJI LA MWANZA KUPITIA STENDI KUU YA MABASI NYEGEZI

    June 10, 2025
  • DC AWATAKA WANANCHI KUSHIRIKI KATIKA UZINDUZI WA MIRADI

    June 02, 2025
  • MHE. MAKILAGI AONGOZA ZOEZI LA USAFI BUHONGWA KATIKA UZINDUZI WA WIKI YA MAZINGIRA

    May 31, 2025
  • Tazama Zote

Video

Ziara
Video Zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Fomu Mbalimbali
  • Kuhusu Sisi

Viunganishi Linganifu

  • Tovuti ya Mkoa wa Mwanza
  • Vibali Kusafiri nje ya Nchi
  • ESS(Watumishi Portal)
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Idara Kuu ya Takwimu(NBS)

Watembeleaji

world map hits counter

Idadi ya wageni

freevisitorcounters's Website

Ramani Elekezi

Wasiliana Nasi

    Barabara ya Balewa

    Sanduku la Posta: 1333,Mwanza

    Simu: +255 28 250 1375

    Simu ya Kiganjani: 0755741738

    Barua Pepe: cd@mwanzacc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Eneo

Copyright ©2017 Mwanza City Council . All rights reserved.