Halmashauri ya Jiji la Mwanza imepokea wageni kutoka halmashauri ya wilaya ya Sumbawanga leo tarehe 21/09/2023 waliofika kwa lengo la kujifunza juu ya shughuli za miradi mbali mbali ya maendeleo na namna ya ukusanyaji mapato ndani ya Halmashauri ya Jiji la Mwanza.
Ugeni huu kutoka sumbawanga umeongozwa na Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Sumbawanga Ndg Gerald Kalolo Ntila akiambatana na Mh. Mbunge, Mkurugenzi wa wilaya hiyo, Waheshimiwa madiwani, Wakuu wa Idara na wataalamu mbalimbali na kupokelewa na Mstahiki Meya wa Jiji la Mwanza.
Akizungumza na wageni hao Mstahiki Meya Ndg. Sima Costantine Sima amewakaribisha wageni hao na kusema, “Nimefurahishwa sana na ujio wenu na ninaamini katika ziara hii kuna mengi mtajifunza pia tutajenga mahusiano mazuri kati ya Halmashauri zetu na kwamba ni sehemu ya refreshment maana Mwanza yetu ina vivutio vingi”. Amesema Ndg. Sima.
Akiwapitisha kwenye mawasilisho ya miradi mbali mbali iliyokamilika na inayoendelea kutekelezwa Ndg. Costantine Luhinda ameeleza miradi kadhaa iliyopo ikiwemo ujenzi wa soko la kisasa,stendi ya mabasi Nyegezi, kiwanda cha tofali,ufugaji wa samaki kwa njia ya cage,uendeshaji wa shule ya English medium, dampo la Kisasa na mingine mingi.Katika kujifunza waheshimiwa madiwani na wataalamu wamepata fursa ya kuuliza maswali mbali mbali na mawsali hayo yamejibiwa kwa kina na wataalamu husika toka Jiji la Mwanza.
Aidha baada ya mawasilisho wageni hao wametembelea mradi wa ujenzi wa soko kuu la kisasa.stendi ya mabasi na ufugaji wa samaki kwa njia ya cage.
Barabara ya Balewa
Sanduku la Posta: 1333,Mwanza
Simu: +255 28 250 1375
Simu ya Kiganjani: 0755741738
Barua Pepe: cd@mwanzacc.go.tz
Copyright ©2017 Mwanza City Council . All rights reserved.