Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Monduli pamoja na wataalamu wametembelea katika Halmashauri ya Jiji la Mwanza leo Januari 9,2025 kwa lengo la kujifunza mambo mbalimbali ikiwemo namna bora ya ukusanyaji wa mapato pamoja na namna ya utekelezaji wa miradi inayomilikiwa na Halmashauri ya Jiji la Mwanza.
Hata hivyo baraza hilo la Madiwani na wataalamu wameambatana na Mkuu wa Wilaya ya Monduli Mhe. Festo Shemswaga na Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo.
Aidha Madiwani pamoja na wataalamu hao wamepata fursa ya kutembelea katika mradi wa ufugaji wa samaki kwa njia ya Vizimba uliopo kata ya Luchelele na kujifunza namna bora ya ufugaji na faida za mradi huo.
Mwisho Baraza la madiwani na wataalamu walipata nafasi ya kutembelea Kisiwa cha Saa nane ili kujionea vivutio na uzuri wa kisiwa hicho kilichopo katikati ya maji katika Ziwa Victoria.
Barabara ya Balewa
Sanduku la Posta: 1333,Mwanza
Simu: +255 28 250 1375
Simu ya Kiganjani: 0755741738
Barua Pepe: cd@mwanzacc.go.tz
Copyright ©2017 Mwanza City Council . All rights reserved.