Mkurugenzi wa Halmashauri ya Ludewa Ndg Sande Deogratias akiwa ameambatana na wataalaamu leo tarehe 03 sep, 2024 amefanya ziara ya kikazi katika Halmashauri ya Jiji la Mwanza kwa Lengo la kujifunza ufugaji wa samaki kwa njia ya vizimba.
Ikiwa Mradi wa ufugaji wa Samaki kwa njia ya vizimba ni moja ya mradi unaofanya vizuri katika miradi ya mpango mkakati iliyopo katika Jiji la Mwanza hivyo wakaona ni vyema kuja kupata elimu ya ufugaji huo wa samaki ili wakautumie katika ziwa Nyasa kwa kufanya uwekezaji mkubwa na wenye tija utakayoiongezea Halmashauri hiyo mapato.
Vilevile wataalamu hao wameweza kufika Eneo la kisoko lililopo Luchelele ambapo uwekezaji wa samaki kwa njia ya vizimba unafanyika ili kupata elimu kutoka kwa Maafsa uvuvi wa Jiji la Mwanza wakiongozwa na Ndg, Suzani ambapo wameeleza zaidi ya vikundi 15 vimenuafaika na wameeleza hatua zote za kufanya mpaka mradi kukamilika ikiwa ni pamoja na kujisajili ili kutambulika na kupewa kibali cha Uvuvi wa samaki kwa njia ya vizimba .
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Ludewa akiwa ameambatana na wataalaamu
Nao wageni kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa wameshukuru kwa ushirikiano na kuahidi yote waliyojifunza wanakwenda kuyafanyia kazi.
Barabara ya Balewa
Sanduku la Posta: 1333,Mwanza
Simu: +255 28 250 1375
Simu ya Kiganjani: 0755741738
Barua Pepe: cd@mwanzacc.go.tz
Copyright ©2017 Mwanza City Council . All rights reserved.