Kamati ya usalama Wilaya ya Nyamagana ikiongozwa na Mwenyekiti wake Mhe, Amina Nassor Makilagi wamefanya ziara ya kukagua Barabara zinazojengwa kwa kiwango cha zege na Mawe mnamo Machi 13,2025
Halmashauri ya Jiji la Mwanza kupitia mapato yake ya ndani hutenga 10% kwa ajili ya ujenzi wa Barabara ambapo zimetengwa shilingi Bilioni 2.5 kwa mwaka wa fedha 2025/2026 kwa ajili ya ujenzi wa Barabara za Mitaa ndani ya Nyamagana.
Mhe Makilagi na kamati yake wamekagua Barabara ya Nyashana iliyopo kata ya Isamilo, vitunguu,Rwagasore, Soko kuu kata ya Pamba, kijereshi kata Mhandu, St.Marry’s kata Igoma,Fumagira kata Kishiri na Ipuli kata ya Mahina na kumtaka mkamdarasi anayesimamia Barabara hizo kuzijenga katika ubora huku akisisitiza nguvu kazi iongezwe ili miundombinu ya Barabara hizo ikamilike kwa wakati.
Naye Mhandisi Datani Kishaka kutoka Tarura ambaye ni msimamizi wa mradi amepokea maelekezo kutoka kwa kamati ya usalama na kuahidi kumaliza Miradi kwa wakati.
Vilevile Kaimu Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza Bw. Jeremiah Lubeleje amesema Halmashauri ipo tayari kutoa fedha za ujenzi wa Miundombinu ya Barabara za Mitaa ili zikamilike kwa wakati uliopangwa.
Mhe Makilagi amesisitiza Miundombinu ya Barabara hizo kukamilika kwa wakati nakueleza kuwa hakutokuwa na muda wa nyongeza.
Barabara ya Balewa
Sanduku la Posta: 1333,Mwanza
Simu: +255 28 250 1375
Simu ya Kiganjani: 0755741738
Barua Pepe: cd@mwanzacc.go.tz
Copyright ©2017 Mwanza City Council . All rights reserved.