Mkufunzi Mkazi Taasisi ya Watu Wazima, Ritta Kakwira akiwa na Afisa Elimu ya Watu Wazima pamoja na Mdhibiti Ubora Jiji, wamefika Gereza la Butimba Mkoani Mwanza kwa lengo la kuhakikisha wanapata makundi wahitaji wa elimu ya Kusoma, Kuhesabu na Kuandika (KKK), Msingi Sekondari pamoja na elimu ya Juu.
Akizungumza mara baada ya kupata makundi hayo Mkufunzi Ritta amesema kuwa kwa sasa wataandaa mpango kazi wa kuanza kutoa elimu hiyo mbadala kwa kutoa Moduli za kumsaidia mfungwa ambaye ni Mwanafunzi kusoma Mwenyewe pamoja na kuandaa walimu watakao wasimamia na kuwaelekeza.
Sambamba na hilo amesema watatoa vitendea kazi kwa ‘material’ Ili kurahisisha kazi ya utoaji wa elimu hiyo nakuifanya kuwa rahisi kwa wafungwa hao kupata elimu ambayo ni haki yao ya kimsingi.
Kwa upande wake Peresi Ngoboka Mkuu wa Kitengo Cha Elimu Gereza Kuu Butimba, ameupongeza Ugeni kutoka kwa Mkurugenzi Wakili Kiomoni Kibamba kwa kufika gerezani hapo kwa lengo la kutatua kero kubwa ya wafungwa ya kutokujua kusoma na kuandika pamoja na wengine kukatisha elimu zao mara baada ya kwenda gerezani.
Ngoboka amesema elimu ya Watu Wazima gerezani hapo italeta haki kwa wafungwa hao ambao bado wanasubiri hatima ya vifungo vyao pamoja na kesi zao, ikiwa ni haki yao ya Msingi kutokana na wengi wao kutojua kusoma na kuandika.
Barabara ya Balewa
Sanduku la Posta: 1333,Mwanza
Simu: +255 28 250 1375
Simu ya Kiganjani: 0755741738
Barua Pepe: cd@mwanzacc.go.tz
Copyright ©2017 Mwanza City Council . All rights reserved.