Halmashsuri ya Jiji la Dodoma yaipongeza Halmashauri ya Jiji la Mwanza kwa hatua iliyofikia katika utendaji wake wa kazi hasa katika ukusanyaji wa mapato, utunzaji wa mazingira na utekelezaji wa Miradi ya maendeleo na ya kimkakati.
Pongezi hizo zimetolewa na Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma Prof. Davis Mwamfupe leo tarehe 30/12/2024 ikiwa ni siku ya kwanza ya ziara ya siku mbili inayojumuisha Madiwani na wataalamu mbalimbali yenye lengo la kujifunza namna ya kubuni na kutekeleza vyanzo vipya vya mapato, utunzaji wa mazingira na namna bora ya utekelezaji wa miradi ya Serikali Kuu katika kuongeza mapato ya Halmashauri.
Akiongea wakati wa kufungua mafunzo hayoNaibu Meya Halmashauri ya Jiji la Mwanza, Bhiku Kotecha amesema,
“Mkiwa Mwanza mtapata fursa ya kuona na kujifunza utekelezaji wa miradi ya kimkakati ikiwemo soko, meli, stendi na daraja la Busisi. Mtaona namna Rais wetu Dkt. Samia Suluhu Hassan amefanya kazi kubwa kukamilisha miradi hii iliyoachwa na muasisi wake, Hayati Dkt. John Pombe Magufuli”
Halmashauri ya Jiji la Mwanza imeendelea kupokea Halmashauri mbalimbali nchini zinazofika kujifunza utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo ya kimkakati.
Itakumbukwa ziara hii imetanguliwa na ziara iliyofanywa na Halmashauri ya Mji wa Nanyamba mkoani Mtwara iliyofika katika Halmashauri ya Jiji la Mwanza kwa ajili ya ziara ya kimafunzo.
Barabara ya Balewa
Sanduku la Posta: 1333,Mwanza
Simu: +255 28 250 1375
Simu ya Kiganjani: 0755741738
Barua Pepe: cd@mwanzacc.go.tz
Copyright ©2017 Mwanza City Council . All rights reserved.