Ikiwa ni siku ya pili ya ziara ya waheshimiwa madiwani na wataalamu wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma katika Halmashauri ya Jiji la Mwanza leomdlu Disemba 31 walipata fursa ya kutembelea baadhi ya Miradi iliyoko ndani na nje ya Halmashauri ya Jiji la Mwanza.
Ziara hiyo iliyoongozwa na Meya wa jiji la Dodoma Prof Davis Mwamfupe imehitimishwa kwa madiwani na wataalamu kutembelea mradi wa ujenzi wa Daraja la Magufuli linalotoka Kigongo Katika Wilaya ya Misungwi kwenda Busisi Wilaya ya Sengerema Mkoani Mwanza.
Akieleza hatua iliyofikiwa Katika mradi huo Mhandisi Mshauri Bw. Aloyce Kadokado amesema,“Mradi huu umefadhiliwa na Serikali yaJamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa asilimia mia moja (100%) na unajengwa na kampuni mbili toka china, Mradi huu umefikia asilimia 94.3% ambapo kufikia February 2025 mradi utakuwa umekamilika ”.
Kadokado ameongeza kuwa mpaka kukamilika kwa mradi huu utagharimu kiasi Tshs Bilioni 716 ambapo mpaka sasa mkandalasi ameshalipwa kiasi cha Tshs Bilioni 434 kati Bilioni 592 bila VAT.
Ameendelea kwa kusema kuwa Hayati John Pombe Magufuli aliuacha mradi ukiwa na asilimia 25% na Mhe Rais wa awamu ya sita Dr. Samia Suluhu Hassan ameendeleza Mradi huu mpaka kufikia asilimia 94.3%.
Aidha Meya wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma Prof. DavisMwamfupe amesema, “ sisi ziara yetu ilihusu kuja kujifunza na kuona kwa macho ya kile kinachoendelea katika utekelezaji wa Miradi,kweli tumeona kwa macho na leo tumepata tafsiri sahihi ya usemi wa Kazi iendelee na kweli inaendelea”.
Naye Bw. Fanuel Kasenene mwakilishi wa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Mwanza aliwashukuru madiwani na wataalamu kutoka Dodoma Jiji kwa kufika na kujionea yale yanayoendelea ndani na nje ya Halmashauri na kuongeza kuwa Mradi huu utaongeza utaongeza pato la Taifa kupitia usafirishaji wa mizigo.
Barabara ya Balewa
Sanduku la Posta: 1333,Mwanza
Simu: +255 28 250 1375
Simu ya Kiganjani: 0755741738
Barua Pepe: cd@mwanzacc.go.tz
Copyright ©2017 Mwanza City Council . All rights reserved.