• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua Pepe |
    • Malalamiko |
Mwanza City Council
Mwanza City Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Jiji la Mwanza

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Orodha ya Viongozi Waliopita
      • Wenyeviti wa Halmashauri
      • Wakurugenzi
      • Wakuu wa Wilaya
    • Dhima na Dira
    • Maadili ya msingi
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Kilimo na Ushirika
      • Maendeleo ya Jamii
      • Uchumi, Mipango na Ufuatiliaji
      • Mazingira na Usafi
      • Fedha na Biashara
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mifugo na Uvuvi
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Maji
    • Vitengo
      • TEHAMA,Habari na Uhusiano
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Sheria na Usalama
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Nyuki
  • Fursa za Uwekezaji
    • Maeneo ya uwekezaji
    • Vivutio vya utalii
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Usafi wa mazingira na uhifadhi wa taka ngumu
    • Leseni
    • Kilimo
    • Mifugo na Uvuvi
    • Maji
  • Baraza la Madiwani
    • Orodha ya madiwani
    • Kamati za kudumu za halmashauri
    • Ratiba ya vikao
    • Mihtasari ya vikao vya baraza
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi inayoendelea
    • TASAF
    • Mfuko wa Jimbo
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu za Maombi
    • Waraka
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Maktaba ya Video
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio Yajayo
    • Magazine

DKT. DUGANGE AFUNGUA MKUTANO MKUU WA 25 WA LVRLAC, AHIMIZA UONGOZI BORA NA ULINZI WA RASILIMALI ZA ZIWA VICTORIA

Posted on: May 26th, 2025

Naibu Waziri wa Ofisi ya Rais – Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI), Mhe. Dkt. Festo John Dugange, amefungua rasmi Mkutano Mkuu wa 25 wa Jumuiya ya Mamlaka za Serikali za Mitaa Kanda ya Ziwa Victoria (LVRLAC) uliofanyika Mei 26, 2025 katika ukumbi wa Kwatunza Beach Resort, Ilemela. Alimwakilisha Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Mashaka Biteko, aliyetoa salamu kwa wajumbe na kueleza kutoweza kuhudhuria kutokana na majukumu mengine ya kitaifa.

Mkutano huo ulihudhuriwa na viongozi wa Serikali, wajumbe wa LVRLAC, wadau wa maendeleo, na wageni waalikwa, ukiwa na kaulimbiu: “Shiriki Uchaguzi Mkuu 2025, Chagua Viongozi Bora.”

Akizungumza wakati wa ufunguzi, Mhe. Dkt. Dugange aliipongeza LVRLAC kwa kuendelea kushirikiana na wadau kama benki ya NMB katika kuandaa mikutano yenye ajenda za maendeleo kwa wakazi wa Ukanda wa Ziwa Victoria. Aliahidi kuwa Serikali kupitia TAMISEMI itaendelea kutoa ushirikiano kuhakikisha rasilimali za Ziwa Victoria zinalindwa na kuendelezwa kwa manufaa ya wananchi.

Pia Mhe. Dkt. Dugange alizihimiza Halmashauri wanachama wa LVRLAC kupitia Mameya/ Wenyeviti na Wakurugenzi kusimamia ipasavyo ukusanyaji wa mapato ya ndani ili ziweze kujitegemea kwa zaidi ya asilimia 80.

Naye Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa Ndugu Fulgence S. Matemele alisisitiza umoja miongoni mwa Halmashauri wanachama na kuwaagiza Wakurugenzi kuhakikisha wanatenga fedha kwa ajili ya malipo ya ada ya mwaka  na kuahidi kushirikiana na uongozi wa LVRLAC katika kuhakikisha kila Halmashauri inalipa michango kwa wakati.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa LVRLAC, Mhe. Willium Gumbo, alisema kwa zaidi ya miaka 20, jumuiya hiyo imekuwa ikijenga uwezo wa Serikali za Mitaa kwa kushirikiana na wadau mbalimbali ili kukuza maendeleo na ustawi wa jamii.

Katibu Mkuu wa LVRLAC, Bw. Billy Albert Brown, alieleza kuwa mkutano huo umeimarisha mshikamano na ushirikiano baina ya Halmashauri wanachama kupitia mikakati madhubuti inayowezesha maendeleo endelevu. Alibainisha kuwa LVRLAC ina kanda tatu – Tanzania, Kenya na Uganda – na kwamba Tanzania inaongoza kwa mafanikio.

Aidha, moja ya ajenda muhimu zilizojadiliwa ni namna ya kutatua changamoto ya magugu maji katika eneo la Busisi–Sengerema, kama sehemu ya majukumu ya LVRLAC ya kulinda usafi wa Ziwa Victoria.

Awali Mhe. Dkt. Dugange alizindua kampeni ya kuhimiza Matumizi ya Nishati Safi ya kupikia pamoja na kugawa majiko kwa Baba lishe na Mama lishe. Kampeni hiyo inaendeshwa na  Mtandao wa Wanawake Viongozi wa LVRLAC.

Matangazo ya Kawaida

  • JITOKEZE KUJIANDIKISHA October 16, 2024
  • TANGAZO LA UPANGISHAJI WA MAENEO YA BIASHARA KATIKA SOKO KUU December 14, 2024
  • UPANGISHAJI WA MAENEO MBALIMBALI YA BIASHARA SOKO KUU May 29, 2025
  • TANGAZO LA MAPENDEKEZO YA SHERIA NDOGO ZA HALMASHAURI YA JIJI LA MWANZA July 10, 2024
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • HANANG' WAJIFUNZA MBINU ZA KUONGEZA MAPATO KUTOKA HALMASHAURI YA JIJI LA MWANZA KUPITIA STENDI KUU YA MABASI NYEGEZI

    June 10, 2025
  • DC AWATAKA WANANCHI KUSHIRIKI KATIKA UZINDUZI WA MIRADI

    June 02, 2025
  • MHE. MAKILAGI AONGOZA ZOEZI LA USAFI BUHONGWA KATIKA UZINDUZI WA WIKI YA MAZINGIRA

    May 31, 2025
  • "SEKTA YA ELIMU HAITAWEZA KUSONGA MBELE KWA MCHANGO WA KUNDI MOJA " , MMHE. MAKILAGI

    May 30, 2025
  • Tazama Zote

Video

Ziara
Video Zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Fomu Mbalimbali
  • Kuhusu Sisi

Viunganishi Linganifu

  • Tovuti ya Mkoa wa Mwanza
  • Vibali Kusafiri nje ya Nchi
  • ESS(Watumishi Portal)
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Idara Kuu ya Takwimu(NBS)

Watembeleaji

world map hits counter

Idadi ya wageni

freevisitorcounters's Website

Ramani Elekezi

Wasiliana Nasi

    Barabara ya Balewa

    Sanduku la Posta: 1333,Mwanza

    Simu: +255 28 250 1375

    Simu ya Kiganjani: 0755741738

    Barua Pepe: cd@mwanzacc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Eneo

Copyright ©2017 Mwanza City Council . All rights reserved.