Madawa ya kulevya ni changamoto na tatizo kubwa kwa binadamu athari zake ni kubwa sana kidiplomasia,kisiasa,kiuchumi na Kijamii pia.
Akizungumza na watumishi wa Halmashauri ya Jiji la Mwanza Leo 28 Novemba 2025. Ndugu Dezidel Tumbu amesema Madawa ya kulevya yapo ya aina mbalimbali kama ya vichocheo ( stimulant ) ambayo ni cocaine,Madawa ya Vipumbaza ambayo ni Heroine pamoja nayoleta Njozi ambayo ni Bangi.
" Dawa za hospitali pia usipozitumia vizuri bila kufata utaratibu wa daktari pia ni Madawa ya kulevya" amesema ndugu Dezidel.
Aidha, kumekuwa na sababu mbalimbali ambazo upelekea mtu kuwa mtumiaji wa Madawa ya kulevya ambazo ni Msongo wa Mawazo,Msukumo lika pamoja na Kuiga Utandawazi.
Sanjari na hayo pia kupo na dalili mbalimbali za mtumiaji wa Madawa ya kulevya ambazo ni Hasira za hovyo,Mabadiliko ya Tabia pamoja na Mabadiliko ya Muonekano.
Lakini pia Madawa ya kulevya yamekuwa na athari mbalimbali kiuchumi,kidiplomasia pamoja na kiusalama pia amesema ndugu Dazidel Tumbu.
Naye John Kaombwe wakili wa kupambana na Madawa ya Kulevya Jijini Mwanza amesema sheria za nchi ni Kali mno kwa anaekamatwa na Madawa ya kulevya ikiwemo ya kifungo gerezani.
Jamii inapaswa kuelewa Madawa ya kulevya ni tatizo na changamoto kwa Taifa yapasa kuepukana na matumizi ya namna hiyo
Barabara ya Balewa
Sanduku la Posta: 1333,Mwanza
Simu: +255 28 250 1375
Simu ya Kiganjani: 0755741738
Barua Pepe: cd@mwanzacc.go.tz
Copyright ©2017 Mwanza City Council . All rights reserved.