Mkuu wa Wilaya ya yamagana Mhe. Amina Makilagi amesema Wilaya yake imefanya vizuri katika kutekeleza miradi ya wananchi kupitia mfuko wa kunusuru kaya maskini (TASAF) kutokana na ushirikiano uliopo baina ya viongozi, wataalamu na wananchi.
Ameyasema hayo katika ziara yake iliyoanza Januari 8 na kuhitimishwa Januari 10,2025 yenye lengo la kukagua miradi inayotekelezwa na TASAF katika kata ya Kishiri,Butimba,Igoma na Mahina na kupokea taarifa za utekelezaji kutoka kwa mratibu wa miradi ya TASAF ngazi ya Halmashauri BW. Kabwe.
Kati ya miradi iliyokaguliwa ni pamoja na ujenzi wa jengo la OPD lenye thamani ya tsh Milioni 140,942,840.10, jengo la IPD lililogharimu tsh 130,684,181.na Thietre tsh 100,045,892.85 katika Zahanati ya Funagila iliyoko kata ya kishili.
Miradi mingine iliyokaguliwa ni jengo la Utawala linalogharimu tsh 100,045,892.85, bweni tsh 160,753,558.14, bwalo tsh 100,045,892.85 na madarasa matatu,Ofisi na matundu 6 ya vyoo vilivyogharimu tsh100,045,892.85 Sekondari ya Nyamagana kata ya Butimba.
Vile vile Mkuu wa Wilaya alikagua mradi wa ujenzi wa mabweni mawili katika shule ya Sekondari Mahina kata ya Mahina yanayogharimu tsh 347,917,290.00.
Pia Makilagi alikagua mradi katika kata ya Igoma ambao ni ujenzi wa mabweni mawili yanayogharimu tsh 349,149,390.00, bwalo tsh 136,945,349.03 pamoja na madarasa matatu,Ofisi na matundu 6 ya vyoo vinavyogharimu tsh132,632,349.03 Shule ya Sekondari Shamaliwa.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya amesema amefurahishwa na miradi ya TASAF katika wilaya yake kwa kufanikiwa kwa kiwango kikubwa na amewapongeza viongozi, kamati na waratibu katika utekelezaji wa majukumu yao.
Aidha amewaomba waendelee kutimiza wajibu wao kwa uadilifu na uaminifu na kuhakikisha kama kuna changamoto wanazitatua ili miradi iweze kukamilika kwa wakati.
Ziara imehitimishwa kwa Mkuu wa Wilaya kufanya mikutano mbalimbali ya hadhara katika kata ya Igogo na Pamba iliyokuwa na lengo la kuhamasisha wazazi kupeleka watoto Shule kwa kuwa Elimu ni haki ya kila mtoto na kutoa agizo kwa viongozi na wasimamizi wa shule kutowawekea masharti yoyote pindi wanapokwenda kuwaandikisha watoto.
Barabara ya Balewa
Sanduku la Posta: 1333,Mwanza
Simu: +255 28 250 1375
Simu ya Kiganjani: 0755741738
Barua Pepe: cd@mwanzacc.go.tz
Copyright ©2017 Mwanza City Council . All rights reserved.