Haya yamesemwa leo na Afisa Maendeleo wa Mkoa wa Mwanza Ndugu Michael Ndasa alipokuwa akizungumza na wadau wa Uvuvi katika ukumbi wa Nyakahoja Jijini Mwanza.
Ndasa amesema ushirikiano mzuri kati ya Vikundi vya Usimamizi wa Rasilimali za Uvuvi(BMU) na viongozi wa serikali kuanzia ngazi ya mtaa ndio Kinga pekee itakayohakikisha usalama wa wavuvi unaimarika ndani ya ziwa Victoria.
Amesema; raiti kama viongozi hao watawajibika ipasavyo vifo vya wavuvi wanaofanya shughuli zao Ziwani havitaripotiwa Kwa wingi kama ilivyo hivi sasa.
Nae Mkurugenzi wa shirika lisilokuwa lakiserikali la EMEDO Bi Edritrudith Lukanga amesema tafiti zinaonesha kuwa watu 236,000 duniani wanakufa Kila mwaka na asilimia 90 ya vifo hivyo vinatokea nchi za Africa.
Akiwasilisha mada yake ya "mitazamo juu ya hatari ya kuzama maji" meneja mradi Ndugu Arthur Mugema amesema shirika la EMEDO limelazimika kufanya utafiti huo wakishirikiana na mashirika ya kigeni ya Ipsos na RNLI ili kupunguza au kuondoa kabisa vifo vitokanavyo na maji ndani ya ziwa Victoria. Amesema makundi mbalimbali ya kijamii yameshiriki katika utafiti huo na majibu yanaonesha kuwa vifo vya maji ni vingi ingawa haviripotiwi.
Akizungumza Kwa niaba ya Mkurugenzi wa Jiji Afisa Uvuvi wa Jiji Ndugu Patrice Justine ameahidi kuvisimamia Vikundi vya BMU na pia kuendelea kutoa elimu zaidi Kwa wavuvi juu ya njia sahihi ya kujilinda ikiwamo kuvaa jaketi za kujilinda (life jackets) wakati wote wawapo Ziwani.
EMEDO wamefanya utafiti huu katika mialo Saba iliyomo ndani ya ziwa Victoria ikiwa ni pamoja na mialo ya Goziba, Ilondo na Musozi iliyoko Ukerewe, na mialo ya Kome na Buseke iliyoko Musoma,mwalo wa Mulumo wa Muleba na pia Mwalo wa Sweya wa Wilayani Nyamagana Jijini Mwanza.
Barabara ya Balewa
Sanduku la Posta: 1333,Mwanza
Simu: +255 28 250 1375
Simu ya Kiganjani: 0755741738
Barua Pepe: cd@mwanzacc.go.tz
Copyright ©2017 Mwanza City Council . All rights reserved.