Ikiwa ni maandalizi ya Mikutano Mkuu wa (ALAT) Taifa Mwenyekiti wa Kamati Tendaji ya Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania (ALAT) Taifa Mhe. Murshid Ngeze amewaongoza wajumbe wa Kamati hiyo katika ziara ya kukagua mradi wa Ujenzi wa Soko kuu la kisasa unayotekelezwa na Serikali katika Halmashauri ya Jiji la Mwanza.
Ziara hiyo imefanyika February 14,2025 kwa lengo la kuona maendeleo na ufanisi wa ujenzi huo na kufanya tathmini ya fursa mbalimbali zitakazopatikana baada ya soko hilo kukamilika.
Aidha Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Jiji la Mwanza Mhe. Sima C. Sima amesema kuwa ahadi ya Serikalini ya awamu ya Sita chini ya Mhe. Rais Dr. Samia Suluhu Hassan inayolenga kutatua adha ya ukosefu wa maeneo ya kufanyia biashara kwa wafanyabiashara, imetimia baada ya Halmashauri ya Jiji la Mwanza kukamilisha ujenzi wa soko kuu la kisasa.
Mhe. Sima ameongeza kuwa Mkandarasi anayetekeleza ujenzi wa soko hili, ni Kampuni ya Mohamed Builders Company L.T.D inayotarajia kukabidhi soko hili hivi karibuni ambapo fursa mbalimbali za kiuchumi zitapatikana na litahudumia zaidi ya wafanyabiashara 1,400.
Naye Msimamizi wa Mradi Bw. Hamis Zakayo amesema kuwa ujenzi umefikia asilimia 99% na inakadiriwa kuwa hadi sasa Serikali imetumia zaidi ya shilingi bilioni 27.
Baada ya ufafanuzi Mwenyekiti wa ALAT Taifa ameongea na vyombo vya habari na kueleza dhana ya Serikali kuanzisha miradi ya kimkakati katika Halmashauri kuwa ni kuijengea uwezo Halmashauri wa kuongeza mapato ya Nchi na kutengeneza msingi wa kujitegemea.
Vile vile Mhe. Ngeze amempongeza mkandarasi kwa kuwa mzalendo na kutekeleza miradi mbalimbali ya Halmashauri kwa kiwango cha juu ambapo katika ujenzi wa Soko kuu la kisasa tayari amefikia asilimia 99% na kuongeza kuwa Halmashauri inao wajibu wa kusimamia vyema na kuendelea kutafuta vyanzo vingine vya mapato ili kujiimarisha kiuchumi.
Mwisho wajumbe hao walipata nafasi ya kutembelea na kukagua ujenzi wa daraja la JPM Kigongo/Busisi, ambalo ujenzi wake umefikia asili.
Barabara ya Balewa
Sanduku la Posta: 1333,Mwanza
Simu: +255 28 250 1375
Simu ya Kiganjani: 0755741738
Barua Pepe: cd@mwanzacc.go.tz
Copyright ©2017 Mwanza City Council . All rights reserved.