Fursa za Uwekezaji zilizopo kwenye sekta ya Mifugo
Halmashauri ya Jiji la Mwanza inaupungufu wa miundombinu ya Mifugo inayofanya kazi kama vile Majosho,Vituo vya kutolea huduma za Mifugo,Malambo,Machinjio n.k.Hivyo Ujenzi wa Miundombinu ya mifugo linaweza kuwa eneo la kipaumbele katika uwekezaji.Maeneo mengine yanayohitajika kwenye uwekezaji ni Uzalishaji wa maziwa na viwanda vya kuongeza thamani ya mazao ya mifugo kama Maziwa,Ngozi na Nyama. Kwenye Sekta ya Mifugo Umelenga Mazao yafuatayo;
Uchakataji wa Nyama
Halmashauri ya Jiji inampango wa kukarabati machinjio yake ya kuchakata nyama kuwa ya kisasa.Kuna uhitaji wa kujenga Machinjio mpya ambayo itaongeza thamani na kulinda soko la ndani la wafugaji
Viwanda vya Ngozi
Kwa kuongeza thamani ya ngozi za wanyama kwa kufanya uchakataji kabla ya kusafirisha nje ya Nchi.
For adding value to the hides and skins by fully processing them or semi processed (wet blue) before export.
Huduma za Mifugo na Madawa
Uanzishwaji wa Maduka ya pembejeo ya Mifugo na vituo vya kutolea huduma za mifugo ambapo Madaktari wa mifugo pamoja na Maafisa Mifugo wanaweza kutoa huduma hasa maeneo ya yasiyofikika kiurahisi.
Barabara ya Balewa
Sanduku la Posta: 1333,Mwanza
Simu: +255 28 250 1375
Simu ya Kiganjani: 0755741738
Barua Pepe: cd@mwanzacc.go.tz
Copyright ©2017 Mwanza City Council . All rights reserved.