Wanufaika wa mikopo itokanayo na asilimia kumi ya mapato ya Halmashauri ya Jiji la Mwanza wamepatiwa mafunzo ya namna ya kufanya biashara zao ili mikopo waliyopatiwa iwe na tija na kuwainua kiuchumi.
Mafunzo hayo yamefanyika katika ukumbi wa mikutano wa Gandhi Hall leo tarehe 30/01/2025 na kuhudhuriwa na wanavikundi waliopata mkopo, Mkuu wa Idara ya Kilimo na Mifugo, Afisa Maendeleo ya Jamii na mwakilishi wa Kitengo cha Mawasilisno Serikalini.
Akifungua mafunzo hayo kwa niaba ya Mkurugenzi Ndg, Erick Mvati ambaye ni Mwenyekiti wa Huduma za mikopo na Mkuu wa Idara ya Kilimo na Mifugo Halmashauri ya Jiji la Mwanza amevipongeza vikundi vyote 87 vilivyokidhi vigezo na kupata sifa ya kupata mkopo wa asilimia 10%ambapo vikundi vya wanawake ni 49, vijana 31 na wenye ulemavu 7 ambavyo vimepatiwa jumla ya Shilingi Bilioni 1.3 kwa wanavikundi wote 488.
Bw. Mvati amesema dhumuni kuu la mafunzo hayo ni kuwajengea uwezo na ufanisi wanufaika wote wa namna ya kusimamia mkopo wa 10% ili kuepuka anguko la kibiashara katika rasilimali zao jambo litakalowawezesha kurejesha na kumaliza mkopo.
Aidha amewataka wanavikundi kuwa waaminifu wakati wa marejesho ukifika kwa kuleta fedha kwa wakati na kiwango kilichopo kwenye mkataba na kuahidi kuwa kwa vikundi vitakavyorejesha mapema vitapata fursa ya kukopeshwa na kupandishiwa kiwamgo cha mkopo kwa awamu nyingine.
Naye Zena Kapama Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Jamii amewaeleza wanufaika wa mkopo kuwa mkopo utarejeswa ndani ya miezi 3 mara baada ya kupokea na kwa vikundi vya ufugaji wa samaki kwa njia ya vizimba watarejesha baada ya miezi nane huku akisema kikundi kinaruhusiwa kulipa zaidi ya rejesho lililoko kwenye mkataba na siyo pungufu na kuwataka kulipa kwa wakati kuepuka usumbufu.
Vilevile amewataka wanufaika kuwa na maelewano katika matumizi ya pesa na kuwasisitiza kutunza akiba ya dharula ili kuepuka usumbufu wakati wa urejeshaji nakuongeza kuwa kikundi kitakachochelewesha kitapewa notisi ya siku 14-30 na wakishindwa sheria itachukua mkondo wake dhidi yao.
Naye Mwenyekiti aliyewawakilisha wanufaika wa mkopo ameishukuru Halmashauri ya Jiji la Mwanza kwa kuwapatia mkopo na amewataka wenzake kuwa Mabarozi wazuri kwa kazi anazozifanya Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe, Dkt. Samia Suluhu Hassani hasa kutoa mkopo na kuahidi kutekeleza vyema ilani ya Chama cha Mapinduzi na kuongeza kuwa mafunzo waliyopata wanakwenda kuyafanyia kazi.
Barabara ya Balewa
Sanduku la Posta: 1333,Mwanza
Simu: +255 28 250 1375
Simu ya Kiganjani: 0755741738
Barua Pepe: cd@mwanzacc.go.tz
Copyright ©2017 Mwanza City Council . All rights reserved.