Kamati ya ushauri ya Wilaya ya Nyamagana DCC, imejadili na kupitisha mapendekezo ya rasimu ya mpango wa bajeti yenye jumla ya kiasi cha Shilingi 124,378,085,328,00 kwa mwaka wa fedha 2025/2026.
Akifungua kikao hicho leo January 31, 2025 katika ukumbi mkubwa wa mikutano Mwakilishi wa Mkuu wa Wilaya Ngd, Thomas James Salala ambaye ni Katibu Tawala wa Wilaya ya Nyamagana amesema lengo la kikao hicho ni kujadili taarifa mbalimbali za utendaji kazi wa Halmashauri kwa ujumla pamoja na kupitisha mapendekezo ya bajeti kwa mwaka wa fedha 2025/2025.
Kikao kimehudhuriwa na Mwakilishi wa Mkuu Wilaya, Kaimu Mkurugenzi,Kamati ya Ulinzi na Usalama Wilaya, Wakuu wa Idara na Vitengo,Viongozi mbalimbali wa Dini, Viongozi wa Vyama Vya Siasa na Wataalamu mbalimbali wa Halmashauri ya Jiji la Mwanza pamoja na Wajumbe mbalimbali.
Katika Kikao hicho , Rasimu ya mapendekezo ya Bajeti imewasilishwa na Mkuu wa Idara ya Mipango na Uratibu Bw. Jeremiah Lubeleje kwa niaba ya Mkurugenzi wa Halmashauri.
Bw. Lubeleje alifafanua kuwa Halmashauri inatarajia kukusanya na kutumia jumla ya Tsh124,378,085,328.00 kwa ajili ya kutekeleza majukumu mbalimbali ikiwemo miradi ya maendeleo na kutoa mchanganuo wa fedha hizo zinazokadiliwa katika Bajeti hiyo kuwa kiasi cha shilingi 83,006,538,000.00 ni fedha ya mishahara ya Watumishi, Kiasi cha Shilingi 2,443,743,000.00 ni matumizi ya kawaida (OC), Kiasi cha Shilingi 6,065,121,084.00 ni Ruzuku ya miradi ya maendeleo, Kiasi cha Shilingi 3,936,058,000.00 ni fedha kutoka kwa wahisani/wadau wa maendeleo na Shilingi 28,926,625,244.00 ni fedha zitokanazo na vyanzo vya Mapato ya ndani ya Halmashauri.
Wajumbe wa kamati wamepata nafasi ya kupitia,kujadili na hatimaye kwa kauli moja wameridhia kupitisha rasimu hiyo ya bajeti kwenda katika ngazi nyingine.
Mwenyekiti wa kikao ambaye ni Katibu Tawala wa Wilaya ya Nyamagana ametamatisha kwa kuwashukuru wajumbe wote kwa kushiriki na kuwapongeza kwa mawazo yao mazuri ya kujenga.
Barabara ya Balewa
Sanduku la Posta: 1333,Mwanza
Simu: +255 28 250 1375
Simu ya Kiganjani: 0755741738
Barua Pepe: cd@mwanzacc.go.tz
Copyright ©2017 Mwanza City Council . All rights reserved.