Ndg. Thomas Aikaruwa Mtaalam wa Mradi - Elimu na Ujuzi kutoka Shirika la Maendeleo la Ujerumani ENABEL, chini ya program ya Green and Smart Cities SASA ameongoza kikao kazi kilichohusisha wajumbe kutoka Manispaa ya Ilemela na Halmashauri ya Jiji la Mwanza katika ukumbi wa Ofisi za Enabel- Mwanza Leo tarehe 08 Julai, 2024
Kikao hicho chenye dhima ya kuanzisha tovuti itakayoshehenezwa taarifa mbalimbali zinazohusiana na masuala ya ukusanyaji taka katika Manispaa ya Ilemela na Halmashauri ya Jiji la Mwanza. Pia kikao hicho kimehusisha washiriki kutoka Idara ya Mazingira, Tehama na Mawasiliano Serikalini.
Akizungumza katika kikao hicho Ndg. Thomas Aikaruwa amesema, "Tovuti hiyo tutakayoianzisha itaonesha taarifa zote za ukusanyaji wa takataka, idadi ya dampo na Mahali zilipo, kujaa kwa dampo husika na aina ya taka zinazokusanywa kwa lengo la kuhakikisha maeneo yote kwa Manispaa ya Ilemela na Halmashauri ya Jiji la Mwanza yanakuwa safi na salama kwa afya ya wananchi wageni na waishio katika maeneo husika".
Akichangia katika kikao hicho Bi. Zamda Gwanko Afisa Tehama Halmashauri ya Jiji la Mwanza amesema kuwa kuna umuhimu wa kuzingatia taratibu zote za eGA ili kupata kibali kitakacho ruhusu tovuti hiyo kuanza kazi rasmi.
Katika kuhitimisha kikao hicho, wajumbe wote wamebaini umuhimu na faida za uwepo wa tovuti hiyo na kuridhika na uanzishwaji wake na kukubaliana kutoa ushirikiano hasa katika upatikanaji wa takwimu za idadi ya mitaa, kata na idadi ya dampo zinazotumika katika kukusanya taka.
Barabara ya Balewa
Sanduku la Posta: 1333,Mwanza
Simu: +255 28 250 1375
Simu ya Kiganjani: 0755741738
Barua Pepe: cd@mwanzacc.go.tz
Copyright ©2017 Mwanza City Council . All rights reserved.