Katika kuboresha na kuongeza ufanisi wa kazi za Maafisa Habari na kuleta mabadiliko chanya katika mawasiliano ndani ya jamii, Aprili 03,2025 Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya mapinduzi Zanzibar, Mhe Hemed Suleiman Abdulla amefungua Kikao Kazi cha 20 cha Maafisa Habari,Mawasiliano, Itifaki na Uhusiano Serikalini katika ukumbi wa Mikutano wa New Amani Hotel Unguja-Zanzibar.
Akifungua Kikao hicho kwa niaba ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi la Zanzibar Mhe Dkt Hussein Ally Mwinyi, Makamu huyo amewataka Maafisa Habari nchini kutoa mrejesho wa kazi zote zinazotekelezwa na Serikali kwa wananchi kuelekea Uchaguzi Mkuu.
"Taarifa za miradi inayotekelezwa na Serikali zote mbili ziwafikie wananchi kwa wakati ili waweze kufanya tathmini ya taarifa za kina za utekelezaji wa miradi ili waweze kufanya maamuzi kuelekea Uchaguzi Mkuu"Amesema Mhe Hemed Suleiman Abdulla.
Mhe. Hemed ameongeza kuwa kikao hicho kina lengo la kutoa mafundo na mazingativu na kujifunza pamoja na Kutoa maelekezo kwa Maafisa Habari wa Tanzania Bara na Zanzibar pamoja na kufanya tathimini kwa kazi zilizofanyika kwa mwaka mzima.
Aidha Mhe Hemed Suleiman Abdulla amewasisitiza Maafisa Habari kuongeza juhudi za kutangaza miradi yote inayotekelezwa na Serikali pamoja na kumuunga mkono Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kazi anazozifanya za kuliongoza Taifa ili kuimarisha utawala bora.
Akihitimisha hotuba yake Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar amesema Serikali itaendelea kukamilisha miradi yote ikiwa ni pamoja na mradi wa Bwawa la Mwalimu Nyerere na Reli ya kisasa ya SGR.
Kikao Kazi hicho kimefunguliwa April 3 na kinatarajia kuhitimishwa Aprili 6,2025.
Barabara ya Balewa
Sanduku la Posta: 1333,Mwanza
Simu: +255 28 250 1375
Simu ya Kiganjani: 0755741738
Barua Pepe: cd@mwanzacc.go.tz
Copyright ©2017 Mwanza City Council . All rights reserved.