Mkuu wa Mkoa wa Mwanza amefunga soko la Mlango Mmoja kutokana na janga la moto lililotokea tarehe 28/09/2018 saa 10:30 alfajiri siku ya Ijumaa.
Akitangaza Agizo hilo la Mkuu wa Mkoa wa Mwanza ,Mkuu wa wilaya ya Nyamagana Mhe.Dkt Phillis Nyimbi amesema wakati huu wanalazimika kufunga soko kwa siku mbili kwa ajili ya wafanyabiashara kuendelea kufanya tathimini ya mali zilizoharibika chini ya vyombo vya ulinzi na usalama.
Aidha Mkuu wa wilaya ya Nyamgana amesema kwa wakati huu Kamati ya Ulinzi na Usalama ya wilaya,Halmashauri ya Jiji la Mwanza, viongozi wa soko,viongozi wa dini pamoja na viongozi wa siasa watakaa pamoja na kuja na mikakati ya muda mfupi,muda wakati na muda mrefu kwa ajili ya soko la Mlango mmoja.
Hata hivyo Dr.Phillis Nyimbi ametoa shukrani kwa wadau wote wakiwemo Polisi, Zima moto,Nile Perch, Mwauwasa pamoja na wananchi walivyojitokeza na kufanya kazi kwa ushirikiano mkubwa uliopelekea moto kudhibitiwa kutokuendelea kuleta madhara makubwa
Moto ulianza kuwaka saa 10:30 Alfajiri ya leo kwenye mabanda ya mama lishe, na mafundi Cherehani na mabanda ya nguo na viatu
Kwa taarifa ya awali ya kamati ya Tathimini imebaini kuwa maduka 23 kati ya 156 yameteketea na Meza 55 kati ya 351 zimetekea zenye mali yenye thamani ya Tsh 583,134,000
Maduka Mengi yalikuwa yakitumika kama stoo ya wafanyabiashara wa Mlango mmoja.
Barabara ya Balewa
Sanduku la Posta: 1333,Mwanza
Simu: +255 28 250 1375
Simu ya Kiganjani: 0755741738
Barua Pepe: cd@mwanzacc.go.tz
Copyright ©2017 Mwanza City Council . All rights reserved.