Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe.John mongella amekabidhi pikipiki 18 zenye thamani ya takribani Tsh 54,000,000 kwa maafisa Elimu wa kata waliomo Katika Halmashauri ya Jiji la Mwanza
Akizungumza kwenye hafla hiyo Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe.John Mongella amewataka Maafisa kuzitumia na kuzitunza vyema kwa lengo lilokusudiwa kwa ajili ya kuleta tija na ufanisi katika sekta ya Elimu.
Aidha Mhe.Mongella amesisitiza kuwa serikali ya awamu ya Tano imejikita kuimarisha sekta ya Elimu, hivyo kila Mwalimu ana wajibu wa msingi wa kuiwezesha sekta hii izidi kusonga mbele kwa kila mwalimu kutimiza wajibu wake “Halmashauri zote 8 za Mkoa wa Mwanza zimepata Pikipiki hizi kwa ajili ya maafisa Elimu Kata hivyo ni imani yangu kuwa vyombo hivi vya usafiri vitaongeza tija na ufanisi katika utendaji wenu wa kazi” alisema Mhe.Mongella.
Akitoa salaam zake Mstahiki meya wa Jiji la Mwanza Mhe.James Bwire amesema wadau wote Jijini Mwanza wanawajibu wa kumuunga mkono Mhe.Dkt John pombe Magufuli kwa kazi kubwa na nzuri anayoifanya ya kuwaletea wananchi maendeleo “Hizi Pikipiki ni sehemu ndogo tu ya kazi inayofanywa na Mhe.Rais,Hivyo ni vyema maafisa elimu kuzitumia pikipiki kwa kazi zilizokusudiwa na si vinginevyo” alisema Mhe Bwire.
Akizungumza katika hafla hiyo,Kaimu mkurugenzi wa Jiji la Mwanza Philipo Kajura Mukama amesema ili kuimarisha usimamizi wa Elimu katika shule zetu Serikali imetoa Pikipiki hizi kwa ajili ya maafisa Elimu wa Kata. Hivyo amewataka maafisa elimu kuzingatia taratibu walizopewa kwa kila mtumiaji wa Pikipiki hizo kuhakikisha anakuwa na leseni inayomruhusu kutumia chombo cha moto.
Hata hivyo Ndugu Mukama amewatahadharisha maafisa elimu kutotumia pikipiki hizo kwa ajili ya kubebea mizigo na Abiria.
Pikipiki hizo zimetolewa na OR-TAMISEMI kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa elimu kupitia programu ya EQUIT na LANES zenye thamani ya Tsh milioni 54
Barabara ya Balewa
Sanduku la Posta: 1333,Mwanza
Simu: +255 28 250 1375
Simu ya Kiganjani: 0755741738
Barua Pepe: cd@mwanzacc.go.tz
Copyright ©2017 Mwanza City Council . All rights reserved.