Akizungumza wakati wa Uzinduzi huo ndugu Marry Tesha Onesmo ameipongoza Ofisi ya Waziri Mkuu,na Ofisi ya Rais Tamisemi kwa Kushirikiana na Wizara ya Mawasiliano kuanzisha zoezi la Uhishaji anuani za Makazi kwa wananchi
Ndugu Marry Tesha ana imani kubwa na Kikosi kazi kilichoundwa na Halmashauri katika kutekeleza zoezi hili kuwa kikosi kazi kitafanya kazi kwa uadilifu ,Umakini na kwa kuzingatia taratibu sheria na kanuni za kazi.
“Ni Imani kuwa zoezi hili likikamilika litaupendezesha Mji wetu wa Mwanza na pia litarahisisha upatikanaji wa huduma mbalimbali za kijamii kama vile suala la ulinzi na usalama,huduma za posta,Tanesco, Zima moto n.k” amesema Mheshimiwa Tesha.
Akizungumza wakati wa uzinduzi huo Mwenyekiti wa kamati ya Kitaifa ya anuani za Makazi NdgMathius Mkoya amesema zoezi hili lilimekwisha anza kwa baadhi ya Majiji na Manispaa hapa nchini na zimefanya vizuri sana .
“Wananchi wamekuwa na Mwitikio mkubwa sana kupata anwani za makazi,zoezi hili limefanya vizuri Dodoma,Arusha na Dar es salaam, ni imani yangu kuwa Mwanza pia mtafanya vizuri’ Amesema ndugu Nkonda.
Aidha Mathius amesema hitaji hili kwa sasa limekuwa ni hitaji la shirika la posta duniani, watu wengi wamekuwa hawatambuliki wanakoishi lakini kwa sasa kupitia zoezi hili kila nyumba na mtaa itapewa namba kwa ajili ya utambulisho
Ndugu Mathius amesema kwa sasa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania imeshaandaa Anuani za Makazi za Mikoa mpaka Kata zote nchini kwa kupewa tarakimu
Barabara ya Balewa
Sanduku la Posta: 1333,Mwanza
Simu: +255 28 250 1375
Simu ya Kiganjani: 0755741738
Barua Pepe: cd@mwanzacc.go.tz
Copyright ©2017 Mwanza City Council . All rights reserved.