Mkuu wa Wilaya ya Nyamgana Ndugu Marry Tesha Onesmo amepiga marufuku wanafunzi kufeli mitihani ya Kidato cha Pili na Cha Nne katika shule zake.
Ndg Marry Tesha Onesmo ameyasema hayo alipokuwa akifanya ziara ya kikazi ya kutembelea na kukagua maendeleo ya kitaaluma ya Shule za Sekondari zilizomo katika wilaya ya Nyamgana .
Licha ya Mkuu wa wilaya kuendelea kutoa pongezi kwa shule za sekondari za wilaya ya Nyamagana kufanya vizuri katika Mitihani ya Kidato cha pili na Kidato cha Nne mwaka 2017 na Kuufanya Mkoa wa Mwanza kuwa watano Kitaifa na Wilaya ya Nyamagana kuwa ya Kwanza Kimkoa.
“Niwapongeze kwa kuendelea kufanya vizuri katika mitihani ya kitaifa na kubakia ndani ya 10 bora kwa kila mwaka licha ya changamoto kadha wa kadha zinazowakabili, na kwa sasa serikali ya awamu ya Tano imeamua kuyatatua”
Ndugu Marry Tesha Onesmo ameendelea kusisitiza kuwa lengo kubwa la serikali ni kuhakikisha wanaboresha elimu na kuzifanya shule za umma kuwa na uwezo wa kushindana na shule za watu binafsi na kuwanufaisha watanzania kwa watoto wao kupata elimu bila malipo.
Suala la nidhamu na utoro wa wanafunzi mashuleni limesisitizwa na Mkuu wa wilaya ya Nyamagana kwa kuwataka wakuu wa shule kuhakikisha watoro wote waliochelewa kwa muda wa mwezi mmoja majina yao kupelekwa kwa maafisa elimu kata na Maafisa hao kuyawasilisha ngazi husika.
Aidha Mkuu wa wilaya amesisitiza Maafisa Elimu Kata kuhakikisha Wanafunzi wote waliofaulu kujiunga na kidato cha Kwanza wanafuatiliwa na kuhakikisha wanadahiliwa kwenye shule husika na kuhudhuria mafunzo na ambao wamejiunga na shule binafsi ni vyema pia ikafahamika ili kuzuia utoro.
Mkuu wawilaya amesema shule ziendelee na ukarabati wa madawati yaliyoaribika ili kuendelea kupunguza changamoto ya upungufu wa madawati
Barabara ya Balewa
Sanduku la Posta: 1333,Mwanza
Simu: +255 28 250 1375
Simu ya Kiganjani: 0755741738
Barua Pepe: cd@mwanzacc.go.tz
Copyright ©2017 Mwanza City Council . All rights reserved.