Mhe Mkuu wa wilaya ya Nyamagana Dkt Phillis Nyimbi amekabidhi Vifaa vya Shule kwa wanafunzi walioathirika na Janga la moto lilotokea Usiku wa Jumatano katika Shule ya Sekondari Mkolani.
Akikabidhi Vifaa hivyo Dkt Nyimbi amesema kama Kamati ya Ulinzi na Usalama ya wilaya wakishirikiana karibu na Kamati ya maafa wameshachukua hatua ya kuunda kikosi kazi cha kuchunguza chanzo cha tukio la moto .
Dkt Phills Nyimbi amesema kinachoshangaza zaidi ni Moto kuunguza Chumba namba 27,37 na 47
Akizungumza Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza Kiomoni Kibamba ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Maafa, amewahasa wanafunzi kutumia vyema miundo mbinu ya Shule hususani vyoo kwa kutotupa taulo za kike ndani ya vyoo suala linalosababisha vyoo kuziba na kupelekea mlipuko wa magonjwa.
Jumla ya Magodoro 12, mashuka 24 madaftari makubwa 60, Kalamu,mafuta na sabuni zimetolewa kwa waanga wa tukio la moto.
Barabara ya Balewa
Sanduku la Posta: 1333,Mwanza
Simu: +255 28 250 1375
Simu ya Kiganjani: 0755741738
Barua Pepe: cd@mwanzacc.go.tz
Copyright ©2017 Mwanza City Council . All rights reserved.