Mhe. Amina Nassoro Makilagi, Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana leo tarehe 27 Jan. 2024 ameongoza shughuli ya upandaji miti katika Shule ya Sekondari Luchelele na Shule ya Msingi Luchelele ambapo jumla ya miti 1,000 ikiwemo ya matunda na ya kivuli imepandwa.
Akizungumza katika Shughuli hiyo ya upandaji miti Mhe. Makilagi amesema, ' Leo tunapanda miti hii ikiwa ni ishara ya kumpongeza Mama yetu Samia Hassan Suluhu ambaye leo ni siku yake ya kuzaliwa. Hivyo badala ya kukata keki sisi tunaungana na watanzania wenzetu kupanda miti ya matunda na ya kivuli. Miti hii itatusaidia kwa matunda na kivuli na pia kupunguza hewa ya ukaa. "
Naye Ndugu Emmanuel Mgimwa kutoka TFS amesema " miti hii ni muhimu kwetu kwani itawasaidia sana watoto wetu. Kwa hiyo nawashauri tuilinde dhidi ya mifugo isiharibiwe. "
Mhe. Makilagi amehitimisha zoezi hili kwa kuwasisitiza wananchi kutoachia mifugo yao hovyo na kuwataka walimu wakuu wa shule hizo kumkabidhi kila mwanafunzi mti uliopandwa autunze siku zote atakazokuwepo shuleni hapo.
Barabara ya Balewa
Sanduku la Posta: 1333,Mwanza
Simu: +255 28 250 1375
Simu ya Kiganjani: 0755741738
Barua Pepe: cd@mwanzacc.go.tz
Copyright ©2017 Mwanza City Council . All rights reserved.