Kamati ya Kudumu ya Bunge OR-TAMISEMI imefanya ziara ya kukagua miradi inayotekelezwa na mpango wa BOOST na SEQUIP mkoa wa Mwanza tarehe 28 oktoba,2023 miradi iliyokaguliwa ni pamoja na mradi wa ujenzi wa shule mpya ya msingi Ng’wang’halanga iliyoko Buhongwa wilayani Nyamagana.
Akifanya majumuisho katika shule hiyo mwenyekiti wa Kamati hiyo Mheshimiwa Justin Nyamoga(MB) amepongeza namna ujenzi ulivyotekelezwa kwa viwango na ubora. Mheshimiwa Nyamoga ameagiza pia halmashauri za mkoa wa Mwanza kuhakikisha wanafanya tathmini ya upungufu wa fedha kwa miradi ambayo haitakamilika kwa upungufu huo na kasha kuwasiliana na wizara ili waongezewe fedha ya kukamilisha mradi kabla ya shule kufunguliwa Januari 2024.Aidha ameagiza wizara yenye dhamana kuhakikisha inawekeza Zaidi kwenye kuboresha vifaa vya kufundishia na kujifunzia ili kutimiza lengo la serikali la kuboresha sekta ya elimu.
Naye Mheshimiwa Deo Ndijembi(MB) kwa niaba ya Naibu waziri wa OR – TAMISEMI amesema kuwa lengo la serikali ni kuhakikisha miradi ya elimu inatekelezeka ili kupunguza msongamano wa wanafunzi darasani pamoja na umbali mrefu wanaotembea kufikia shule zilipo.kadhalika mheshimiwa Ndijembi ameahidi kuwa serikali ya awamu ya sita itaendelea kuleta fedha ili kutekeleza miradi hii ikiwemo pia miradi ya afya,maji na miundo mbinu ya bara bara.
Nao wajumbe wa kamati hiyo ya Bunge wakati wa majumuisho yao wamepongeza namna nzuri ambavyo shule ya msingi Ng’wang’halanga imepangiliwa na kuishauri serikali kupanga maeneo na kuyatunza kwa ajili ya ujenzi wa shule nyingine baadaye kwa kuwa idadi ya watu inazidi kuongezeka siku hadi siku sambamba na hayo viongozi wa mkoa wa Mwanza kupitia Mheshimiwa Amina Makilagi Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana ambaye pia amemuwakilisha mkuu wa mkoa wa Mwanza amepokea salamu za pongezi zilizotolewa na kamati na kuahidi kusimamia maagizo yote yaliyotolewa.
Barabara ya Balewa
Sanduku la Posta: 1333,Mwanza
Simu: +255 28 250 1375
Simu ya Kiganjani: 0755741738
Barua Pepe: cd@mwanzacc.go.tz
Copyright ©2017 Mwanza City Council . All rights reserved.