Mhe. Stanslaus Mabula Mbunge wa Nyamagana amefanya ziara leo Julai 9, 2024 katika Kata ya Pamba kutekeleza ahadi ya kukabidhi madawati katika shule za Sekondari.
Mbunge wa Nyamagana, ametembelea shule mbili kati ya nne zilizopo kata ya Pamba ambazo ni Mlimani Secondary na Bugarika Sekondari ambapo shule hizo zimepewa madawati 50 kila moja ili kupunguza changamoto ya wanafunzi kukaa chini na kuwatengenezea mazingira rafiki ya kujisomea.
Vilevile Mhe.Stanslaus Mabula Mbunge wa Nyamagana ameeleza kuwa takribani milioni 30 zimetengwa kwa mwaka huu wa fedha 2024/2025 kwa ajili ya manunuzi ya madawati, Viti, na meza nakuongeza kuwa zitatumika pia kuboresha miundombinu ikiwa ni kujenga na kuboresha ya zamani ili iendane na ya kisasa.
Naye,Mkuu wa shule ya Sekondari Bugarika Ndg.Zacharia Miyeye amempongeza Mbunge na Serikali kwa ujumla kwa kuwapatia madawati kwani wana jumla ya wanafunzi 1331 na upungufu wa madawati 540 nakusema kuwa hayo madawati 50 yaliyoletwa yatasaidia kupunguza chamgamoto iliyopo nakuongeza kuwa mipira waliyopatiwa itawawezesha wanafunzi kukuza vipaji vyao.
Mbunge huyo wa Nyamagana amehitimisha kwa kuahidi kuwa serikali itaendelea kuboresha sekta ya Elimu kwa kutumia fedha za mfuko wa Jimbo, Fedha kutoka Serikali kuu na za mapato ya ndani ya Halmashauri ili kuweka mazingira rafki kwa wanafunzi kujisomea.
Barabara ya Balewa
Sanduku la Posta: 1333,Mwanza
Simu: +255 28 250 1375
Simu ya Kiganjani: 0755741738
Barua Pepe: cd@mwanzacc.go.tz
Copyright ©2017 Mwanza City Council . All rights reserved.