Baraza la Madiwani Halmashauri ya Wilaya ya Buchosa wamepata mafunzo juu ya namna bora ya ukusanyaji wa mapato na ufugaji wa samaki kwa njia ya vizimba.
Mafunzo hayo yametolewa na wataalamu wa Halmashauri ya jiji la Mwanza wakati wa Ziara ya kikazi ya Baraza la madiwani na wataalamu kutoka Buchosa leo Disemba 6, 2024.
Akifungua mafunzo hayo yaliyofanyika katika ukumbi mkubwa Kaimu Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza Bw. Erick Mvati ameeleza vyanzo mbalimbali vya mapato vilivyoiburiwa na Halmashauri ya Jiji la Mwanza kwa lengo la kuhakikisha mapato yanakusanywa ya ya kutosha ili kutekeleza Miradi ya maendeleo.
Kwa upande mwingine Baraza hilo limepata Elimu juu ya ufugaji wa samaki kwa njia ya vizimba ambapo limefanikiwa kufika eneo la ufugaji katika kata ya Luchelele na kukutana na wataalamu pamoja na wanufaika wa mradi huo.
Mmoja wa wanufaika wa mradi huo Bw.Fikiri Elias amesema mradi huo umewasadia vijana wengi kujiajiri ambapo kupitia mazao ya Samaki wanapata faida inayowasaidia kujikimu kimaisha pamoja na kuchangia pato la Nchi.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Buchosa Mhe.Idama Kibanzi amempongeza Kaimu Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza pamoja na watendaji wote kwa kuweza kushirikiana vyema katika kukuza mapato ya Jiji pamoja na usimamizi na utekelezaji mzuri wa miradi huku akiahidi kwenda kufanyia kazi yote waliyojifunza.
“Kipekee naomba kutoa shukrani zangu za dhati kabisa kwa mapokezi mazuri kutoka kwenu na pia kujitoa kwenu kutupatia Elimu hii ya ukusanyaji wa kodi na utekelezaji wa Miradi, Hakika ziara yetu imekua yenye mafanikio makubwa kwani tumejifunza mambo mengi na mazuri na tutayafanyia kazi pindi tutakaporejea Buchosa“Amesema Mhe. Kibanzi.
Katika hatua nyingine Madiwani wametoa shukrani za dhati kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Buchosa kwa kuandaa ziara hiyo ya mafunzo ya ukusanyaji wa mapato ya ndani kupitia vyanzo mbalimbali na namna ya usimaiaji wa miradi ya kimkakati inayotekelezwa kwenye Halmashauri hizo.
Kwa kuhitimisha kaimu Mkurugenzi Bw. Mvati alilishukuru Baraza la madiwani na wataalamu toka Buchosa kwani ujio wao unalenga kuendeleza mahusiano mazuri baina ya Halmashauri hizo lakini pia kujiimarisha katika utendaji.
Barabara ya Balewa
Sanduku la Posta: 1333,Mwanza
Simu: +255 28 250 1375
Simu ya Kiganjani: 0755741738
Barua Pepe: cd@mwanzacc.go.tz
Copyright ©2017 Mwanza City Council . All rights reserved.