Kuelekea katika kilele cha maadhimisho ya wiki ya utumishi wa Umma, halmashauri ya Jiji la Mwanza imefanya maadhimisho hayo katika viwanja vya Nyamagana. Katika siku hii watumishi na wananchi wamefanikiwa kufika na kupata huduma mbalimbali na vile vile kuwajulisha jinsi ambavyo Halmashauri imejipanga katika kuhakikisha dhuduma nyingi zinapatikani kwa njia ya kidigitali. Pia tumefanikiwa kufanya bonanza na matamasha mbalimbali. Pia kufikia usiku tulifanikiwa kuwasikiliza viongozi mbalimbali wa Wilaya ya Nyamagana na Halmashauri ya Jiji kwa Jinsi walifanikisha shughuli mbalimbali na jinsi ambavyo walivyojipanga kwa ajili ya mwaka wa fedha 2024/2025Mwitikio umekuwa mzuri na tunawashukuru sana wananchi na watumishi waliofanikiwa kufika na kutembelea maonesho hayo katika viwanya hivi vya Nyamagana.
Barabara ya Balewa
Sanduku la Posta: 1333,Mwanza
Simu: +255 28 250 1375
Simu ya Kiganjani: 0755741738
Barua Pepe: cd@mwanzacc.go.tz
Copyright ©2017 Mwanza City Council . All rights reserved.