Kamati ya Fedha na uongozi ya Halmashauri ya Jiji la Mwanza imefanya ziara ya kikazi kukagua utekelezaji wa miradi ya Afya, Elimu na Uchumi inayotekelezwa na Halmashauri kwa kutumia mapato ya ndani.
Miradi iliyotembelewa ni pamoja na Ujenzi wa jengo la abiria katika kiwanja cha ndege cha Mwanza, ujenzi wa sehemu za kutembelea na uwekaji wa umeme katika kituo cha Afya cha Igoma, Ujenzi wa wadi ya wanaume Hospitali ya wilaya ya Nyamagana, Ujenzi wa soko la muda la Mbugani pamoja na Ujenzi wa madarasa saba shule ya Sekondari ya pamba.
Akizungumza baada ya kuhitimisha ziara hiyo Mstahiki meya wa Jiji la Mwanza Mhe. James Bwire amesema kama kamati wameridhika na kasi ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo unaoendelea kwa mwaka wa fedha 2019/2020.
" Ninampongeza Mkurugenzi na timu yake ya watalaam kwa kazi nzuri wanayoendelea kuifanya kwa kutekeleza miradi kwa kadri tunavyoagiza kwenye vikao vyetu.
At a hivyo Mhe. Bwire amewahaidi wafanyabiashara wa Soko la muda la mbugani kushughulikia changamoto walizonazo za mitaro na kuwekewa mapaa kwenye soko la Kuku na Soko la mkunguni.
Barabara ya Balewa
Sanduku la Posta: 1333,Mwanza
Simu: +255 28 250 1375
Simu ya Kiganjani: 0755741738
Barua Pepe: cd@mwanzacc.go.tz
Copyright ©2017 Mwanza City Council . All rights reserved.