Jiji la Mwanza kujenga miradi mikubwa ya Soko la Kisasa na Stendi ya Mabasi
Posted on: July 26th, 2019
Halmashauri ya Jiji la Mwanza, leo Julai 25 imetiliana saini ya ujenzi wa soko la kisasa na Stendi ya kisasa na mkandarasa wa kampuni ya ujenzi ya Mohammed Buildings ambayo ni kampuni ya kizawa yenye makao makuu yake mkoani Tanga. Kampuni hiyo ya kizawa itafanya kazi chini ya mkandarasi mshauri kampuni ya OMG ambayo ilibuni na kuchora ramani ya stendi ya Msamvu ya Morogoro. Ujenzi wa soko la kisasa na Stendi hiyo ya kisasa ambao unatarajia kuanza muda wowote kuanzia Sasa, utagharimu Sh. bilioni 38 na ujenzi wake utafanyika kwa miezi 15.
Kuanza kwa ujenzi huo kunatajwa kutaongeza ukuaji wa uchumi wa jiji la Mwanza pamoja na kuongeza pato la Taifa.
Pia ujenzi wa vitega uchumi hivyo katika jiji hilo ambalo ni kubwa kwa mikoa kanda ya ziwa na miongoni mwa majiji yanayochangia kiasi kikubwa cha pesa kwenye pato la Taifa.
Pamoja na hayo ujenzi wa vitega uchumi hivyo katika halmashauri ya Jiji la Mwanza ni utekelezaji wa ahadi ya Rais John Magufuli wakati wa kampeni mwaka 2015 kwamba, "jiji la Mwanza kuwa kama jiji la Calfonia".
Pia pesa za ujenzi wa soko na Stendi hiyo zimetolewa na serikali kuu kwa kila halmashauri zilizokidhi vigezo vya kuandika andi