Mstahiki Meya wa Jiji la Mwanza Ndg. Sima Costantine Sima kwa niaba ya Wananchi, Madaktari na Wauguzi wa Hospitali ya Wilaya ya Nyamagana Jijini Mwanza, amepokea vifaa tiba kutoka Jiji la Wurzburg nchini Ujerumani tarehe 01 Desemba,2023 vyenye thamani ya shilingi milioni 115. kwa ajili ya huduma ya wodi ya Watoto wachanga (Neonatal) ikiwa ni matokeo mazuri ya mahusiano mema yaliyopo kati ya Mji wa Mwanza na Mji wa Wurzburg- Ujerumani.
Awali kabla ya makabidhiano hayo, Mganga Mkuu wa Hospitali ya wilaya ya Nyamagana Dkt. Pima Sebastian alieleza kuwa Hospitali hiyo haikuwa na Kitengo maalum cha huduma kwa ajili ya Watoto wachanga hivyo kwa kushirikiana na Jiji Rafiki la Wurzburg- Ujerumani waliona vema kuanzisha rasmi kitengo hicho na hivyo kufanikisha kupata vifaa tiba ambavyo ni:- Ultrasound 2, Babywormers 5, na vifaa vingine muhimu kwa ajili ya wodi ya Watoto.
Aidha Dkt. Pima amesema “ Madaktari Pamoja na wauguzi 40 watapatiwa mafunzo ya namna nzuri ya kutumia vifaa hivyo ambapo madaktari na wauguzi 20 tiyari wamepata mafunzo hayo na wengine 20 watapatiwa mafunzo pia ili kwa Pamoja huduma hii kwa Watoto iweze kuboreka Zaidi.”
Kwa upande wake Ndg. Billy Brown ambaye ni Mratibu wa Miji Dada katika Halmashauri ya Jiji la Mwanza ameeleza furaha kubwa aliyonayo kwa mahusiano mazuri kati ya Jiji la Mwanza na Jiji la Wurzburg yaliyoanza tangu mwaka 1966 na kwamba kupitia mahusiano hayo miradi mingi imetekelezeka ukiwemo sasa huu wa vifaa tiba kwa ajili ya wodi ya Watoto wachanga katika hospitari yetu ya wilaya ya Nyamagana.
Akihitimisha shughuli hiyo ya mapokezi ya vifaa tiba hospitalini hapo, Mstahiki Meya Ndg. Sima ametoa shukrani za dhati kwa niaba ya Wananchi na Madaktari wa Wilaya ya Nyamagana kwa Meya wa Jiji la Wurzburg Ndg. Christian Schuchardt akiwakilishwa na Ndg. Dominick Weshofern na Bi. Anuschka Heid kwa kuona umuhimu juu ya jambo hili muhimu; huku akiwataka madaktari na wauguzi hospitalini hapo kuvitumia na kuvitunza vema vifaa hivyo ili viendelee kutufaa Zaidi kwa mahitaji ya huduma za Watoto wachanga.
Barabara ya Balewa
Sanduku la Posta: 1333,Mwanza
Simu: +255 28 250 1375
Simu ya Kiganjani: 0755741738
Barua Pepe: cd@mwanzacc.go.tz
Copyright ©2017 Mwanza City Council . All rights reserved.