Waziri mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Kassim Majaliwa, Majaliwa ameipongeza Halmashauri ya Jiji la Mwanza Kwa usimamizi mzuri wa Fedha za serikali.
Mheshimiwa Kassim Majaliwa ameyasema hayo jana alipofanya ziara ya kikazi Katika Wilaya ya Nyamagana.
Waziri Mkuu yupo Mkoani Mwanza kwa siku saba kwa ajili ya kukagua miradi mbali mbali ya maendeleo inayotekelezwa na serikali sambamba na hilo waziri Mkuu yupo kuelezea musimamo na muelekeo wa serikali ya awamu ya tano kwa watumishi wa umma.
“ Katika kupitia makabrasha yangu na vyanzo vyangu vya taarifa nimejiridhisha Nyamagana mpo salama” amesema Mheshimiwa Majaliwa alipofanya kikao cha pamoja na watumishi wa umma ukumbi wa BOT. Mwanza
Aidha Waziri Mkuu ameendelea kusisitiza nidhamu, uwajibikaji na uadilifu kwa watumishi wa umma kwa kusema kuwa serikali ya awamu hii haipo tayari kuunda Tume kwa mtumishi yeyote ambaye wamejiridhisha sio muadilifu wala muaminifu kwa fedha za serikali.
Mheshimiwa Majaliwa amewahaidi watumishi wote wa umma kuwa na subira kwani serikali inatambua changamoto mbalimbali zinazowakabili watumishi wa umma hususani suala la maslahi ambapo kwa sasa serikali imeunda tume ya mishahara na Motisha kwa watumishi ambayo inashughulika na maslahi ya mishahara kwa kila kada.
Pamoja na Hilo, Mheshimiwa Majaliwa amewataka waheshimiwa Madiwani pamoja watendaji kuwa utengemano wa pamoja katika kubaini vyanzo vya mapato na kuvisimamia ili kuweza kutekeleza miradi mbali mbali ya maendeleo kwa wananchi.
Akiwasilisha taarifa ya Wilaya ya Nyamgana, Mkuu wa wilaya ya Nyamagana amesema Halmashauri yake imekusanya kiasi cha zaidi ya Bilioni Tano mpaka mwezi Desemba 2017, na kufikia asilimia 56 ya makusanyo yote kwa mwaka 2017/18, wametoa mikopo ya vijana na akina mama zaidi ya milioni 160 kwa mwaka 2017/18, zaidi ya asilimia 82 ya wakazi mjini wanapata maji, wanaviwanda vikubwa zaidi ya 74 , wamerasimisha viwanja zaidi ya 19000
Mheshiwa Majaliwa amehitimisha ziara yake kwa kufungua Zahanati ya bulale- Buhongwa yenye thamani zaidi ya Milioni 200,pamoja na ugawaji wa kadi za matibabu kwa wazee wa wilaya ya Nyamagana
Barabara ya Balewa
Sanduku la Posta: 1333,Mwanza
Simu: +255 28 250 1375
Simu ya Kiganjani: 0755741738
Barua Pepe: cd@mwanzacc.go.tz
Copyright ©2017 Mwanza City Council . All rights reserved.