Afisa mwandikishaji wa Jimbo la Nyamagana Kiomoni Kibamba afungua mafunzo kwa maafisa waandikishaji wa Daftari la kudumu la mpiga kura
Posted on: August 10th, 2019
Afisa mwandikishaji wa Jimbo la Nyamagana Kiomoni Kiburwa Kibamba amefungua mafunzo kwa Maafisa wa uboreshaji wa Daftari la kudumu la mpiga kura ( BVR kit operators) na waandishi wasaidizi , Semina hiyo imefanyika katika Ukumbi wa Sokoine Chuo cha Ualimu Butimba na Shule ya Sekondari Ngaza .
Akizungumza katika ufunguzi huo, Afisa wa Jimbo la uchaguzi la Nyamagana Kiomoni Kibamba amewapongeza maafisa hao kwa kuaminiwa na kuchaguliwa kuifanya kazi kubwa ya kitaifa ya uboreshaji wa Daftari la kudumu la mpiga kura.
Aidha Mkurugenzi amewataka maofisa hao kuwa wasikivu na kuzingatia mafunzo watakayopewa kwa siku mbili kuhusiana na uendeshaji wa zoezi hilo.
Hata hivyo Kibamba amesema hawatamvumilia mtu yoyote atakayekuwa mzembe wakati wa uboreshaji wa Daftari.
" Kama Nyamagana tunataka tuwe watu wa kwanza kitaifa kuandikisha watu wengi zaidi na hii inawezekana tukiwa na weledi na tukizingatia mafunzo tutakayopewa" Amesema Kibamba.
Zoezi la uboreshaji Daftari la kudumu la mpiga kura linatarajia kuanza mapema Agosti 13 na kufikia tamati yake tarehe 19 wilayani Nyamagana