• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua Pepe |
    • Malalamiko |
Mwanza City Council
Mwanza City Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Jiji la Mwanza

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Orodha ya Viongozi Waliopita
      • Wenyeviti wa Halmashauri
      • Wakurugenzi
      • Wakuu wa Wilaya
    • Dhima na Dira
    • Maadili ya msingi
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Kilimo na Ushirika
      • Maendeleo ya Jamii
      • Uchumi, Mipango na Ufuatiliaji
      • Mazingira na Usafi
      • Fedha na Biashara
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mifugo na Uvuvi
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Maji
    • Vitengo
      • TEHAMA,Habari na Uhusiano
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Sheria na Usalama
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Nyuki
  • Fursa za Uwekezaji
    • Maeneo ya uwekezaji
    • Vivutio vya utalii
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Usafi wa mazingira na uhifadhi wa taka ngumu
    • Leseni
    • Kilimo
    • Mifugo na Uvuvi
    • Maji
  • Baraza la Madiwani
    • Orodha ya madiwani
    • Kamati za kudumu za halmashauri
    • Ratiba ya vikao
    • Mihtasari ya vikao vya baraza
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi inayoendelea
    • TASAF
    • Mfuko wa Jimbo
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu za Maombi
    • Waraka
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Maktaba ya Video
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio Yajayo
    • Magazine

WAJUMBE WA MABARAZA YA KATA WATAKIWA KUTIMIZA WAJIBU WAO KWA HAKI

Posted on: March 26th, 2025

Katika jitihada za kuhakikisha utendaji kazi wa Mabaraza ya kata unaimarika maeneo mbalimbali ya Halmashauri ya jiji la Mwanza, leo Machi 26,2025 Wenyeviti, makatibu na wajumbe 131 wameapishwa na kukumbushwa majukumu yao.

Hafla hiyo imefanyika katika ukumbi mkubwa wa Jiji na kuhudhuriwa na Maafisa Sheria wa Halmashauri ambao kabla ya kuwaapisha wajumbe waliwaelimisha namna ya kutekeleza majukumu yao kwa kuzingatia sheria, taratibu na kanuni za usuluhishi katika mabaraza ili kumaliza migogoro katika jamii.

Awali Bw. Nobert John Sospeter Afisa Sheria, aliwakumbusha wajumbe juu ya sheria za uundaji wa Mabaraza ya Kata, muundo, sifa za mtu kuwa mjumbe wa Baraza pamoja na kuwakumbusha majukumu ikiwa ni namna ya utekelezaji wa majukumu hayo.

Aidha Wakili Mwandamizi wa Serikali Richard Vungwa alipata nafasi ya kuwaapisha wajumbe hao na kuwataka kutenda haki wakati wakitimiza majukumu yao kwa kuzingatia miongozo.

Wakili Vungwa aliitaja migogoro itakayoshughulikiwa na Mabaraza hayo kuwa ni pamoja na migogoro ya ndoa na migogoro ya ardhi.

Sambamba na hilo amewataka wajumbe kuwa wasuluhishi na siyo waamuzi,kwani kwa mujibu wa Sheria ya Mahakama ya Migogoro ya Ardhi sura ya 216, mabaraza ya kata yanasikiliza Migogoro na kusuluhisha na ikishindikana baraza litatoa hati ya kushindikana usuluhishi wa mgogoro kwa hatua zaidi.

Mabaraza ya kata ni vyombo vilivyoundwa kwa mujibu wa kifungu cha 3 cha Sheria ya mabaraza ya kata ya mwaka 1985, ambapo kila baraza linajumuisha wajumbe wasiopungua wanne na wasiozidi wanane watakaochaguliwa na kamati ya kata kutoka miongoni mwa majina ya wakazi wa kata yaliorodheshwa kwa kuzingatia taratibu maalum uliowekwa.

Matangazo ya Kawaida

  • TANGAZO KWA WAOMBAJI AMBAO HAWAJAWASILISHA TAARIFA ZAO KWA AJILI YA MNADA April 30, 2025
  • JITOKEZE KUJIANDIKISHA October 16, 2024
  • TANGAZO LA UPANGISHAJI WA MAENEO YA BIASHARA KATIKA SOKO KUU December 14, 2024
  • TANGAZO LA KUPEWA NA KUINGIZWA KATIKA MFUMO WA TAUSI -UPANGISHAJI WA SOKO KUU MWANZA February 21, 2025
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • WAKILI KIBAMBA ASISITIZA NIDHAMU ENEO LA KAZI

    May 08, 2025
  • WAWEZESHAJI WATOA MBINU ZA UFUNDISHAJI WA SOMO LA KIINGEREZA KUONGEZA UFAULU NYAMAGANA

    May 05, 2025
  • WAJUMBE WA MABARAZA YA KATA WATAKIWA KUTIMIZA WAJIBU WAO KWA HAKI

    March 26, 2025
  • DC NYAMAGANA MTAA KWA MTAA KUSIKILIZA KERO ZA WANANCHI

    March 28, 2025
  • Tazama Zote

Video

Maadhimisho ya wiki ya utumishi wa Umma Halmashauri ya Jiji la Mwanza
Video Zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Fomu Mbalimbali
  • Kuhusu Sisi

Viunganishi Linganifu

  • Tovuti ya Mkoa wa Mwanza
  • Vibali Kusafiri nje ya Nchi
  • ESS(Watumishi Portal)
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Idara Kuu ya Takwimu(NBS)

Watembeleaji

world map hits counter

Idadi ya wageni

freevisitorcounters's Website

Ramani Elekezi

Wasiliana Nasi

    Barabara ya Balewa

    Sanduku la Posta: 1333,Mwanza

    Simu: +255 28 250 1375

    Simu ya Kiganjani: 0755741738

    Barua Pepe: cd@mwanzacc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Eneo

Copyright ©2017 Mwanza City Council . All rights reserved.