• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua Pepe |
    • Malalamiko |
Mwanza City Council
Mwanza City Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Jiji la Mwanza

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Orodha ya Viongozi Waliopita
      • Wenyeviti wa Halmashauri
      • Wakurugenzi
      • Wakuu wa Wilaya
    • Dhima na Dira
    • Maadili ya msingi
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Kilimo na Ushirika
      • Maendeleo ya Jamii
      • Uchumi, Mipango na Ufuatiliaji
      • Mazingira na Usafi
      • Fedha na Biashara
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mifugo na Uvuvi
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Maji
    • Vitengo
      • TEHAMA,Habari na Uhusiano
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Sheria na Usalama
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Nyuki
  • Fursa za Uwekezaji
    • Maeneo ya uwekezaji
    • Vivutio vya utalii
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Usafi wa mazingira na uhifadhi wa taka ngumu
    • Leseni
    • Kilimo
    • Mifugo na Uvuvi
    • Maji
  • Baraza la Madiwani
    • Orodha ya madiwani
    • Kamati za kudumu za halmashauri
    • Ratiba ya vikao
    • Mihtasari ya vikao vya baraza
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi inayoendelea
    • TASAF
    • Mfuko wa Jimbo
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu za Maombi
    • Waraka
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Maktaba ya Video
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio Yajayo
    • Magazine

MLIPUKO WA KIPINDUPINDU MWANZA, WANANCHI WATAKIWA KUCHUKUWA TAHADHARI.

Posted on: January 9th, 2024



Kamati ya Afya ya Msingi ya Jiji la Mwanza imejadili juu ya suala la mlipuko wa ugonjwa wa kipindupindu ulio ripotiwa na Daktari Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana Dr. Pima Sebastian siku ya tarehe 9 Januari,, 2024 katika ukumbi wa Halmashauri ya Jiji la Mwanza.

Akitoa taarifa ya uwepo wa ugonjwa huo wa kipindupindu katika kikao hicho kilicho jumuisha wadau mbalimbali kama  MWAUWASA, TARURA, TMDA, Watendaji wa kata, na baadhi ya  wenyeviti,  Daktari Pima amesema " Mnamo tarehe 04 Januari, 2024 tumepokea wagonjwa wawili wenye  dalili za ugonjwa wa kipindupindu ambao walitokea Mkoa jirani wa Simiyu ambako walienda kwa shughuli za msiba. Walianza kusikia dalili za  kuharisha na walipofika Igoma walipokelewa katika Zahanati ya Igoma na kuchukiliwa sampuli nazo zilibainika kuwa na ugonjwa huo baadaye walipelekwa katika kituo cha matibabu kilichopo mkuyuni."

Aidha, amesema kuwa zimeendelea kulipotiwa taarifa za visa vingine vya ugonjwa huo viwili toka eneo la Mkolani, vitatu Wilaya ya jirani ya Ilemela na hadi sasa  kuna jumla ya wagonjwa 7 waliolazwa na wawili wameruhusiwa  wanaendelea vizuri.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa wenyeviti Ndg. Abubakar Ameshauri kuwa taarifa hizi za mlipuko wa kipindupindi zisambazwe  ziwafikie wananchi kupitia mitandao ya  kijamii kwenye makundi ya wenyeviti, watumishi, wanamichezo, na watumishi wasio wa umma.

Naye Mhe. Diwani wa kata ya igoma Ndg. Musa Ngolo amesisitiza  kuwa elimu ya njia sahihi ya kujikinga na kipindupindu itolewe bila kuyasahau makundi maalumu kama   wasio sikia na wasio ona pia kuwepo na mawasiliano ya haraka toka eneo husika waliko patikana wagonjwa ili hatua za haraka zichukuliwe ili kuzuia maambukizi zaidi. 


 Mwenyekiti  wa kamati ya Afya  ya Msingi kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana,  Ndg.  Thomas James Salala amesisitiza kuwa taarifa zianze kutolewa mara moja kwa jamii  juu ya uwepo wa ugonjwa huu kupitia vyombo vya habari, matangazo ya barabarani, na vikao vya mitaa ili kuhamasisha watu namna ya kujikinga kwa pamoja tuepukane na mlipuko huu wa ugonjwa wa kipindupindu.

Matangazo ya Kawaida

  • TANGAZO KWA WAOMBAJI AMBAO HAWAJAWASILISHA TAARIFA ZAO KWA AJILI YA MNADA April 30, 2025
  • JITOKEZE KUJIANDIKISHA October 16, 2024
  • TANGAZO LA UPANGISHAJI WA MAENEO YA BIASHARA KATIKA SOKO KUU December 14, 2024
  • TANGAZO LA KUPEWA NA KUINGIZWA KATIKA MFUMO WA TAUSI -UPANGISHAJI WA SOKO KUU MWANZA February 21, 2025
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • WAKILI KIBAMBA ASISITIZA NIDHAMU ENEO LA KAZI

    May 08, 2025
  • WAWEZESHAJI WATOA MBINU ZA UFUNDISHAJI WA SOMO LA KIINGEREZA KUONGEZA UFAULU NYAMAGANA

    May 05, 2025
  • WAJUMBE WA MABARAZA YA KATA WATAKIWA KUTIMIZA WAJIBU WAO KWA HAKI

    March 26, 2025
  • DC NYAMAGANA MTAA KWA MTAA KUSIKILIZA KERO ZA WANANCHI

    March 28, 2025
  • Tazama Zote

Video

Maadhimisho ya wiki ya utumishi wa Umma Halmashauri ya Jiji la Mwanza
Video Zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Fomu Mbalimbali
  • Kuhusu Sisi

Viunganishi Linganifu

  • Tovuti ya Mkoa wa Mwanza
  • Vibali Kusafiri nje ya Nchi
  • ESS(Watumishi Portal)
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Idara Kuu ya Takwimu(NBS)

Watembeleaji

world map hits counter

Idadi ya wageni

freevisitorcounters's Website

Ramani Elekezi

Wasiliana Nasi

    Barabara ya Balewa

    Sanduku la Posta: 1333,Mwanza

    Simu: +255 28 250 1375

    Simu ya Kiganjani: 0755741738

    Barua Pepe: cd@mwanzacc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Eneo

Copyright ©2017 Mwanza City Council . All rights reserved.