• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua Pepe |
    • Malalamiko |
Mwanza City Council
Mwanza City Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Jiji la Mwanza

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Orodha ya Viongozi Waliopita
      • Wenyeviti wa Halmashauri
      • Wakurugenzi
      • Wakuu wa Wilaya
    • Dhima na Dira
    • Maadili ya msingi
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Kilimo na Ushirika
      • Maendeleo ya Jamii
      • Uchumi, Mipango na Ufuatiliaji
      • Mazingira na Usafi
      • Fedha na Biashara
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mifugo na Uvuvi
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Maji
    • Vitengo
      • TEHAMA,Habari na Uhusiano
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Sheria na Usalama
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Nyuki
  • Fursa za Uwekezaji
    • Maeneo ya uwekezaji
    • Vivutio vya utalii
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Usafi wa mazingira na uhifadhi wa taka ngumu
    • Leseni
    • Kilimo
    • Mifugo na Uvuvi
    • Maji
  • Baraza la Madiwani
    • Orodha ya madiwani
    • Kamati za kudumu za halmashauri
    • Ratiba ya vikao
    • Mihtasari ya vikao vya baraza
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi inayoendelea
    • TASAF
    • Mfuko wa Jimbo
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu za Maombi
    • Waraka
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Maktaba ya Video
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio Yajayo
    • Magazine

MKAKATI TOKOMEZA KIPINDUPINDU MWANZA, MSISITIZO WAWEKWA KATIKA USAFI WA MAZINGIRA.

Posted on: January 25th, 2024

Mkuu wa wilaya ya Nyamagana Mhe.Amina Nassoro Makilagi leo tarehe 25/01/2024 ameongoza kikao mkakati cha kutokomeza mlipuko na maambukizi mapya ya ugonjwa wa kipindupindu katika ukumbi mkubwa wa Halmashauri ya jiji la Mwanza, kilicho jumuisha Mganga Mkuu wa Serikali, wakuu wa Idara mbalimbali ndani ya Jiji, walimu wakuu Shule za Msingi na Sekondari, Watendaji wa Kata na Mitaa, maafisa afya, maendeleo ya jamii, wataalam wa kilimo, mifugo na uvuvi, na kamati ya usalama ya Wilaya.

Akifungua kikao hicho Mhe. Makilagi amesema " Lengo kubwa leo tufanye  tathimini ili tujuwe tangu ugonjwa wa kipindupindu umeanza hadi sasa hali ikoje na kwamba kufikia tarehe 27/01/2024 pasiwepo ugonjwa huu tena. " Amesema Mhe. makilagi.

Akitoa tathimini hiyo kwa niaba ya Daktari wa Wilaya Ndugu Sophia Kiluvya ambaye ni Afisa Afya wilayani hapa amesema kuwa tangu ugonjwa huu umeingia wilayani Nyamagana  tumepokea wagonjwa 66. Wagonjwa 06 wakiwa wametokea Wilaya jirani na wagonjwa 60 kutoka wilaya  ya Nyamagana. Ambapo hadi sasa wagonjwa 62 wameruhusiwa , wawili (02), na wawili walifariki.

Mhe. Makilagi amemkaribisha Mganga mkuu wa serikali profesa. Nagu katika kikao hicho huku akimshukuru kwa kuwa tayari kufika mwanza hasa katika  kipindi hiki cha mlipuko wa ugonjwa wa kipindupindu kuwatia moyo wauguzi lakini pia kushauri ili kusaidia kuzuia ugonjwa huu Nyamagana  na Mkoa wa Mwanza kwa ujumla.

Kwa upande wake Profesa. Nagu ameshukuru kuwa sehemu ya kikao hicho na kuwasilisha salaam za pongezi kwa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza na watendaji wake wote hasa sekta ya Afya kwa kutoa huduma nzuri kwa wagonjwa na kuhakikisha  Afya zao zinaendelea kuboreka.

Profesa Nagu amesema "Ugonjwa wa kipindupindu ni ugonjwa wa uchafu hivyo sisi watumishi tuhakikishe maeneo yetu ya makazi , biashara  maeneo ya kazi  na mazingira yote kwa ujumla  ni safi ili vimelea  vya ugonjwa huu visiendelee kukua, na mitaro yote yenye changamoto izibuliwe pamoja  na maeneo ya wavuvi na jamii kwa ujumla.

Aidha Profesa Nagu amewasihi watumishi wote kuhakikisha wanahamasisha usafi na matumizi sahihi ya vyoo pamoja na kuweka miundombinu  bora katika maeneo ya vyoo ili kila mtu anapomaliza kupata huduma ya haja ndogo na kubwa anawe mikono kwa maji tiririka na sabuni.

Akihitimisha kikao  hicho Mhe. Makilagi amesema kuwa kutokana na mikakati hii na maelekezo haya, mtaa    utakao ripotiwa  kuwa bado una ugonjwa wa kipindupindu baada ya tarehe 27/01/2024 kila anayehusika katika eneo hilo ataandika barua ya mistari mitatu(3) akieleza kwa nini yeye aendelee kuwa mtumishi wa serikali ya Tanzania.

Matangazo ya Kawaida

  • TANGAZO KWA WAOMBAJI AMBAO HAWAJAWASILISHA TAARIFA ZAO KWA AJILI YA MNADA April 30, 2025
  • JITOKEZE KUJIANDIKISHA October 16, 2024
  • TANGAZO LA UPANGISHAJI WA MAENEO YA BIASHARA KATIKA SOKO KUU December 14, 2024
  • TANGAZO LA KUPEWA NA KUINGIZWA KATIKA MFUMO WA TAUSI -UPANGISHAJI WA SOKO KUU MWANZA February 21, 2025
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • WAKILI KIBAMBA ASISITIZA NIDHAMU ENEO LA KAZI

    May 08, 2025
  • WAWEZESHAJI WATOA MBINU ZA UFUNDISHAJI WA SOMO LA KIINGEREZA KUONGEZA UFAULU NYAMAGANA

    May 05, 2025
  • WAJUMBE WA MABARAZA YA KATA WATAKIWA KUTIMIZA WAJIBU WAO KWA HAKI

    March 26, 2025
  • DC NYAMAGANA MTAA KWA MTAA KUSIKILIZA KERO ZA WANANCHI

    March 28, 2025
  • Tazama Zote

Video

Maadhimisho ya wiki ya utumishi wa Umma Halmashauri ya Jiji la Mwanza
Video Zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Fomu Mbalimbali
  • Kuhusu Sisi

Viunganishi Linganifu

  • Tovuti ya Mkoa wa Mwanza
  • Vibali Kusafiri nje ya Nchi
  • ESS(Watumishi Portal)
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Idara Kuu ya Takwimu(NBS)

Watembeleaji

world map hits counter

Idadi ya wageni

freevisitorcounters's Website

Ramani Elekezi

Wasiliana Nasi

    Barabara ya Balewa

    Sanduku la Posta: 1333,Mwanza

    Simu: +255 28 250 1375

    Simu ya Kiganjani: 0755741738

    Barua Pepe: cd@mwanzacc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Eneo

Copyright ©2017 Mwanza City Council . All rights reserved.