• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua Pepe |
    • Malalamiko |
Mwanza City Council
Mwanza City Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Jiji la Mwanza

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Orodha ya Viongozi Waliopita
      • Wenyeviti wa Halmashauri
      • Wakurugenzi
      • Wakuu wa Wilaya
    • Dhima na Dira
    • Maadili ya msingi
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Kilimo na Ushirika
      • Maendeleo ya Jamii
      • Uchumi, Mipango na Ufuatiliaji
      • Mazingira na Usafi
      • Fedha na Biashara
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mifugo na Uvuvi
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Maji
    • Vitengo
      • TEHAMA,Habari na Uhusiano
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Sheria na Usalama
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Nyuki
  • Fursa za Uwekezaji
    • Maeneo ya uwekezaji
    • Vivutio vya utalii
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Usafi wa mazingira na uhifadhi wa taka ngumu
    • Leseni
    • Kilimo
    • Mifugo na Uvuvi
    • Maji
  • Baraza la Madiwani
    • Orodha ya madiwani
    • Kamati za kudumu za halmashauri
    • Ratiba ya vikao
    • Mihtasari ya vikao vya baraza
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi inayoendelea
    • TASAF
    • Mfuko wa Jimbo
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu za Maombi
    • Waraka
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Maktaba ya Video
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio Yajayo
    • Magazine

"Hatua na muendelezo huu ni mzuri kwa ujenzi wa miradi hii ya Soko na Stendi " Mhe Mwanaidi Ali Khamis

Posted on: January 9th, 2021

"Nimeridhishwa na kasi ya ujenzi pamoja na vifaa vya kisasa vinavyotumika kwenye ujenzi huu" Mhe Mwanaidi Ali Khamis

Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Mwanaidi Ali Khamis ametoa kauli hiyo Januari 09.2021 akiwa kwenye ziara ya siku moja katika Halmashauri ya Jiji la Mwanza  kukagua mradi mkakati wa ujenzi  wa Soko Kuu uliopo Kata ya Pamba katika Halmashauri ya Jiji la Mwanza utakaogharimu Shilingi Bilioni 23


Mhe. Khamis akiwa ameambatana na wenyeji wake Dkt. Philis Nyimbi Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana na kamati yake ya Ulinzi na usalama,  amekagua ujenzi wa soko Hilo la Kisasa uliofikia 8% ya ujenzi wake na kuridhishwa na telnolojia yenye mitambo  ya kisasa inayotumiwa na mkandarasi mzawa wa kampuni ya ujenzi ya Mohammed Builders.


Aidha Mhe. Khamis ameagiza Mkandarasi Mshauri kuweka usimamizi wa mradi huo kwa masaa 24 sanjari na kutoa siku mbili kwa Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana kushirikiana na Halmashauri ya Jiji la Mwanza kusimamia Mkandarasi aweke mpango madhubuti wa utatuzi wa uhaba wa Saruji ili mradi huo ukamilike kwa wakati.


Akiongea kwa niaba ya wananchi wa Jimbo la Nyamagana Mhe. Stanslaus Mabula ameishukuru serikali ya Dkt. John Pombe Magufuli kutoa fedha ili mradi huo utekelezwe ambao ujenzi wake ulisitishwa kwa taratibu kadhaa za kiserikali takribani mwaka mmoja ambao ulileta adha kwa wananchi wanaohitaji huduma pamoja na wafanyabiashara na wachuuzi wa Soko Hilo.

Mstahiki Meya  wa halmashauri Jiji la Mwanza Mhe. Sima Constantine Sima akiwa ameambatana na wataalamu wa Jiji wakiongozwa na Mkurugenzi wa Jiji  Kiomoni Kibamba, kwaniaba ya  Halmashauri Jiji la Mwanza ameahidi kuendelea kusimamia vyema miradi mikakati yote inayotekelezwa katika halmashauri yake ambayo itachochea ukuaji wa Jiji la Mwanza pamoja uongezaji wa mapato wa halmashauri ili ijiendeshe yenyewe. Wakati huo huo Mhe. Ngoye  Diwani Kata ya Pamba ambaye pia Ni Naibu Mayor ameishukuru serikali kwa ujenzi wa Soko hilo katika Kata yake ya Pamba ambao umesogezea wananchi wake huduma karibu na kuleta unadhifu wa mji.

Naye Mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya ujenzi ya Mohammed Builders  kampuni ya Kizawa iliyoshinda Zabuni ya ujenzi huo amesema anakutana na wakati mgumu wa utekelezaji wa mradi huo kutokana na uhaba wa Saruji japo Kama analipa fedha kwa wakati viwandani. Hivyo ameiomba serikali itafute namna Bora ya utatuzi wa uhaba huo ili miradi huweze kukamilika kwa wakati.

Matangazo ya Kawaida

  • TANGAZO KWA WAOMBAJI AMBAO HAWAJAWASILISHA TAARIFA ZAO KWA AJILI YA MNADA April 30, 2025
  • JITOKEZE KUJIANDIKISHA October 16, 2024
  • TANGAZO LA UPANGISHAJI WA MAENEO YA BIASHARA KATIKA SOKO KUU December 14, 2024
  • TANGAZO LA KUPEWA NA KUINGIZWA KATIKA MFUMO WA TAUSI -UPANGISHAJI WA SOKO KUU MWANZA February 21, 2025
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • MHE. MAKILAGI AONGOZA ZOEZI LA USAFI BUHONGWA KATIKA UZINDUZI WA WIKI YA MAZINGIRA

    May 31, 2025
  • "SEKTA YA ELIMU HAITAWEZA KUSONGA MBELE KWA MCHANGO WA KUNDI MOJA " , MMHE. MAKILAGI

    May 30, 2025
  • MCHENGERWA AWATAKA MAAFISA HABARI KUWA WABUNIFU

    May 23, 2025
  • DKT. DUGANGE AFUNGUA MKUTANO MKUU WA 25 WA LVRLAC, AHIMIZA UONGOZI BORA NA ULINZI WA RASILIMALI ZA ZIWA VICTORIA

    May 26, 2025
  • Tazama Zote

Video

Ziara
Video Zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Fomu Mbalimbali
  • Kuhusu Sisi

Viunganishi Linganifu

  • Tovuti ya Mkoa wa Mwanza
  • Vibali Kusafiri nje ya Nchi
  • ESS(Watumishi Portal)
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Idara Kuu ya Takwimu(NBS)

Watembeleaji

world map hits counter

Idadi ya wageni

freevisitorcounters's Website

Ramani Elekezi

Wasiliana Nasi

    Barabara ya Balewa

    Sanduku la Posta: 1333,Mwanza

    Simu: +255 28 250 1375

    Simu ya Kiganjani: 0755741738

    Barua Pepe: cd@mwanzacc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Eneo

Copyright ©2017 Mwanza City Council . All rights reserved.