Naibu waziri wa Maji na Uwamagiliaji Mhe. Jumaa Aweso akiwa na mwenyeji wake Mhe. Stanslaus Mabula Mbunge Jimbo la Nyamagana amebanisha hayo, Kata ya Igoma akihutubia wananchi katika mkutano wa hadhara.h
Mhe. Aweso amesema, wizara yake imeandaa mradi mpya wa waji utakaowezesha ujenzi wa Chanzo Kipya cha Maji Butimba chenye uwezo wakuhudumia takribani wakazi 400,000 ili kuondoa kabisa uhaba wa maji wilayani humo kwa takribani miaka 20 ijayo. Kadharika amewasihi wananchi wa Nyamagana waendelee kuunga mkono jitihada kubwa za serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli imejidhatiti kutatua changamoto ya uhaba wa maji na kuoneshabkwa vitendo dhamira ya dhati kumtua Ndoo mwanamke kichwami.
Wakati huo huo Mkurugenzi wa MWAUWASA *Mamlaka ya Maji safi na Taka na Usafi wa mazingira Mkoani Mwanza* Mhandishi. Antony Sanga, amewahakikishia wananchi wa Nyamagana na viungia vyake hususani maeneo ya pembezoni kuwa ipo miradi mitano mikubwa inatekelezwa hivi sasa yenye lengo la kukabiliana na changamoto ya uhaba wa maji ikiwemo mradi unaogharimu Tsh. 17.89 BIL na mkandarasi yupo kazini kupitia kampuni ya kichina *CCECC* China Civil Engineering Constration Corporation, Mradi utakao kamilika ifikapo mwaka 2020 ili kutoa huduma kata ya Igoma
na ukanda wa Kishiri, Luchelele, Lwanimah, Buhongwa, Nyegezi pamoja na wilaya Magu eneo la Kisesa Magu, Ilemela pamoja na eneo la Usagara wilayani Misungwi.
Naye Mbunge wa Nyamagana Mhe. Stanslaus Mabula amewaambia wananchi wa Nyamagana takribani miaka 30 kilijengwa chanzo kimoja cha Maji cha Capripont kuhudumia watu 108,000 na kwasasa kina hudumia wilaya mbili Nyamagana na Ilemela ambapo kwa wakazi wa Nyamagana pekee hakitoshi. Lakini ndani ya uongozi wake ameweka historia mpya itakaoweka Msingi imara kwa utatuzi wa maji miaka 20 ijayo. Vile vile Mhe. Mabula amewahakikishia wana Nyamagana kuwatumikia kwa dhati kuhakikisha ahadi zote zilizotolewa kwenye Ilani ya Uchaguzi zinatekelezeka ikiwemo upatikanaji wa maji safi na salama ya uhakika.
Mkutano huo wa hadhara umehudhuriwa nadiwani mwenyeji Mhe. Musa Magabe, Mhe.mudogo
Barabara ya Balewa
Sanduku la Posta: 1333,Mwanza
Simu: +255 28 250 1375
Simu ya Kiganjani: 0755741738
Barua Pepe: cd@mwanzacc.go.tz
Copyright ©2017 Mwanza City Council . All rights reserved.