Mhe. Amina Nassoro Makilagi Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana ameongoza shughuli za Usafi wa Mazingira na upandaji miti katika eneo la kata ya Buhongwa; hususani katika Shule ya Msingi Bulale na Shule ya Msingi Amina Makilagi zilizopo katika kata ya Buhongwa leo tarehe 08/12/2023 ikiwa ni zoezi maalum kuelekea siku ya Kihistoria, siku ya Uhuru nchini Tanganyika yaani Tanzania kwa sasa.
Akizindua zoezi la Upandaji miti Mhe, Makilagi amewaeleza Wananchi, viongozi na Wanafunzi wa maeneo hayo kuwa “Lengo la zoezi hili ni kutukumbusha sisi Watanzania na sisi wana Nyamagana wapi tulipo toka, wapi tulipo na wapi tunakoelekea na hivyo asije akatokea mtu akavuruga Amani na Uhuru tulioupata.”
Naye Wakala wa Misitu kutoka TFS Ndg. Emmanuel Mgimwa amesema kuwa miti iliyotolewa ni pamoja na miti ya matunda, mbao na miti ya urembo. Ameitaka jamii ya kata hiyo kutoa ushirikiano wa kutosha ili kuhakikisha miti hiyo inakuwa na kufikia malengo na matarajio mema ya upandaji miti hiyo.
Mhe. Makilagi amehitimisha kwa kuwashukuru TFS kwa kutoa miti hiyo, wananchi, na Wanafunzi kwa ujumla kwa kushiriki zoezi muhimu la upandaji miti na kusema kuwa tunalojukumu kubwa kuhakikisha miti hiyo tuliyoipanda inakua na kuwa faida kwetu maana tukiitunza miti hiyo itatutunza.
Barabara ya Balewa
Sanduku la Posta: 1333,Mwanza
Simu: +255 28 250 1375
Simu ya Kiganjani: 0755741738
Barua Pepe: cd@mwanzacc.go.tz
Copyright ©2017 Mwanza City Council . All rights reserved.