HALMASHAURI YA JIJI LA MWANZA YAPOKEA VIFAA KINGA- UVIKO-19
Uongozi wa Aga Khan Foundation Development (AFD) kupitia hospitali ya Aga Khan Mkoa wa Mwanza wamekabidhi vifaa kinga kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Mwanza Bw. Seleman Yahaya Sekiete kukabiliana na ugonjwa wa UVIKO-19 katika ofisi za halmashauri ya jiji hilo leo Jumatatu tarehe 16 Agosti 2021.
Akikabidhi vifaa hivyo Mganga Mfawidhi wa hospitali ya Aga Khan Dkt Bernardin Ngaila amesema kuwa taasisi imetoa vifaa kinga vikiwemo Gloves za kawaida za kushikia wagonjwa, (Disposable Surgical Face Masks) Face Shield,Barakoa (Examination Face Masks) na N95 Masks vyenye thamani ya Shilingi Millioni ishirini na tano laki nane na tisini elfu
Akipokea vifaa hivyo Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Mwanza Bw.Seleman Yahaya Sekiete, ametoa shukrani za dhati kwa taasisi hiyo na kuahidi kuvitumia kikamilifu vifaa hivyo katika vituo vya Afya ili kukabiliana na wimbi la tatu la ugonjwa wa UVIKO-19.
Aidha taasisi zote mbili zimetoa shukrani za dhati na pongezi kwa serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Mhe.Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa jitihada kubwa katika kukabiliana na janga la UVIKO-19.
Kaimu Mganga mkuu wa jiji akitoa maelezo ya vifaa kinga vya UVIKO-19 kwa Mkurugenzi wa jiji
.Picha na Martin Sawema.
Barabara ya Balewa
Sanduku la Posta: 1333,Mwanza
Simu: +255 28 250 1375
Simu ya Kiganjani: 0755741738
Barua Pepe: cd@mwanzacc.go.tz
Copyright ©2017 Mwanza City Council . All rights reserved.